Songwe Ndege ya kwanza yatua Uwanja wa kimataifa

Ndege ya kwanza kutua katika uwanja wa kimataifa wa Songwe Mkoani Mbeya ikijaza mafuta, baada ya ujenzi wa  uwanja huo kukamilika na kuanza kazi rasmi jana.Picha na Brandy Nelson

Muktasari:

“Tumeanzisha historia mpya kwani dunia inafahamau kwa sasa kuna uwanja wa kimataiafa wa Songwe, upo wazi umekamilika na umeanza kutumika rasmi leo(jana),”alisema
Alisema kuwa uwanja wa Songwe wa kimataifa ni kati ya viwanja vikubwa viwili kujengwa baada ya uhuru ukitanguliwa na uwanja wa Mkoa wa Kilimanjaro kwani viwanja vingine vimekuwa vikifanyiwa marekebisho.

HATIMAYE Ndege ya kwanza ya abiria imetua katika Uwanja wa kimataifa wa Songwe jana baada ya miaka 11 ya ujenzi wake ambao tayari umekamilika na kugharimu Sh100 bilioni.

Akizungumza baada ya kutua ndege hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege Tanzania (TAA), Seleman Seleman alisema kuwa tayari uwanja wa kimataifa wa Songwe umekamilika na dunia nzima ina taarifa ya kukamilika kwa uwanja huo.

Alisema kuwa kutokana na kukamilika kwa uwanja huo, tayari ofisi za mamlaka hiyo imeshahamia katika uwanja huo na kuanza shughuli zake rasmi huku uwanja wa zamani ukifungwa rasmi na hakuna ndege yoyote itakayoweza kutua katika uwanja huo.

“Tumeanzisha historia mpya kwani dunia inafahamau kwa sasa kuna uwanja wa kimataiafa wa Songwe, upo wazi umekamilika na umeanza kutumika rasmi leo(jana),”alisema
Alisema kuwa uwanja wa Songwe wa kimataifa ni kati ya viwanja vikubwa viwili kujengwa baada ya uhuru ukitanguliwa na uwanja wa Mkoa wa Kilimanjaro kwani viwanja vingine vimekuwa vikifanyiwa marekebisho.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Deodatus Kinawiro alisema, aliwataka wananchi wa Mkoa wa Mbeya kujiandaa kutumia uwanja huo kwa kuongeza kipato chao na kuinua uchumi wa mkoa.

Alisema kuwa wakazi wa Mbeya wanapaswa kuzalisha kwa wingi maua na matunda kwa nia ya kuinua uchumi. wa mkoa huo na uweze kukua, “Tusiutumie uwanja huu kwa lengo la kusafiria pekee”alisema na kuongeza:

“Uwanja wa Songwe ni fursa muhimu kwa wakazi wa Mkoa wa Mbeya na mikoa jirani, kwani utaweza kuwasaidia katika kuongeza pato la mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla kutokana na uwanja huo kuwa wa kimataifa ambapo shughuli mbali mbali za kiuchumi zitafanyika kutokana na uwanja huo,”alisema.