MwanzoContactsEmail
Home Kazi
BOOKMARK THIS PAGE
Kikwete: Takrima ngumu kuikwepa  Send to a friend
Friday, 14 May 2010 22:07

*ASEMA K’LIMANJARO HUWEZI KUWAITA WAZEE BILA KITOCHI CHA MBEGE
Fredy Azzah
RAIS Jakaya Kikwete amesema utekelezaji wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi hasa katika kipengele kinachokataza takrima, ni mgumu.

 Rais Kikwete alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na viongozi wa dini katika semina ya siku mbili iliyoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na kufanyika katika Hoteli ya WhiteSands jijini Dar s Salaam.

“Tumeendelea kuboresha Sheria ya Gharama za Uchaguzi, lakini, lile la takrima ni gumu. Mfano katika mkoa wa Kilimanjaro huwezi kuwaita wazee ukazungumza nao bila kitochi,” alisema Kikwete.

Kitochi ni kipimo cha lita moja ya pombe ya kienyeji aina ya mbege inayotengenezwa mkoani Kilimanjaro.

Rais aliendelea kusema “Wakati wa kampeni mwaka 2005 nilifika mahali wakawa wananiambia, mzee hili ni jambo la kawaida hata Chadema, CUF wakija wanafanya hivi, hiyo ni sehemu muhimu kwao, huwezi kuwaita wazee bila mbege.”

Katika kuthibitisha kauli yake hiyo Rais Kikwete alimtaka mmoja wa maaskofu wanaotoka Kanda ya Kaskazini kueleza endapo inawezakana kuwaita wazee wa mkoa huo bila kitochi.

Askofu huyo ambaye jina lake halikufahamika mara moja, alimjibu Kikwete "Kwa kweli hili haliwezekani. Hiyo ni sehemu ya maisha ya watu wa Kilimanjaro."

Baada ya jibu hilo la askofu, ukumbi mzima akiwa Rais Kikwete mwenyewe ulilipuka kwa kicheko na baadaye rais aliendelea kuzungumza na viongozi hao bila kusema nini kifanyanyike ili sheria hiyo iweze kutekelezeka maeneo kama hayo.
Kwa mujibu wa Rais Kikwete kabla ya kutungwa kwa Sheria hii mpya ya Gharama za Uchaguzi, hali ilikuwa mbaya kiasi kwamba kabla ya mtu kufikiria kugombea, alianza kufikiri kwanza jinsi ya kupata fedha za kununua watu ili wampitishe kwenye kura za maoni.

“Mwende mkawahubirie watu kuwa wawachague watu wenye nia njema, watakaoweza kuliendeleza taifa, msiengemee chama chochote na pia tuendelee kukumbushana kuyakubali matokeo,” aliagiza Rais Kikwete.
Katika hatua nyingine, Rais Kikwete pia alitumia fursa hiyo kuwaonya viongozi hao juu ya tabia inayoanza kujitokeza ya dini moja kuikejeli dini nyingine.

Alisema ingawa Tanzania ina uhuru wa kuabudi, pale dini yoyote itakapofanya kitendo hicho hadharani, serikali itaingilia kati.

“Wengine wanasema kuwa tunaingilia uhuru wa kuabudu, lakini siyo kweli, sisi sheria zetu zinasema usikejeli dini ya mwenzako, ukifanya hivyo sisi tunaingilia kati,” alisema Kikwete.

Kikwete pia alisisitiza umuhimu wa kushirikiana  kati ya viongozi wa dini na serikali akieleza kuwa pande hizo zote zina lengo moja la kutaka upendo na maendeleo kwa jamii.
Alisema wakati mwingine serikali inaweza kufanya jambo ambalo kwa namna moja au nyingine linaweza kuwakera viongozi hao wa dini na kuwa hali hiyo itakapotokea, viongozi hao wasisite kuwasiliana naye moja kwa moja au kupitia mawaziri.

“Sisi wote ni binadamu kwa hiyo tutaweza kukosea lakini, nyie mna watu, unaweza kumwambia waziri au mtu mwingine amwambie waziri mkuu kuwa mnataka kuonana naye au aniambie mimi.Pia mnaweza kutumia simu yangu iko wazi muda wote unaweza kunipigia uniambie moja kwa moja,” alisisitiza Kikwete.

Awali Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Iringa Dk Owdemburg Mdegella alisema kikao hicho kimepitisha maazimio saba ambayo pande zote mbili; serikali na viongozi wa dini wamekubali kuyatekeleza.

“Kwa kuwa Serikali imeona umuhimu wa kutayarisha Sheria ya Gharama za Uchaguzi na kuwashirikisha viongozi wa dini ili kuielewa, kuijadili na kuifikisha kwa waumini; viongozi wa dini tunapongeza na kuhimiza serikali kuwa waaminifu katika kuitekeleza,” alisema Askofu Dk Mdegella.

Alisoma maazimio hayo kuwa ni serikali kuweka utaratibu maalum wa kukutana na viongozi wa dini mara mbili kwa mwaka na Serikali kudumishe utaratibu wa kutumia mtandao wa viongozi wa dini kwa kupanua wigo wa ushiriki ili kufikisha taarifa sahihi kwa jamii yote.

Maazimio mengine ni viongozi wa dini washirikishwe mapema katika hatua za awali wakati wa kushughulikia masuala mbalimbali muhimu ya kitafa na viongozi wa dini wasishabikie siasa katika nyumba za ibada.

Kwa mujibu wa Askofu Mdegella maazimio mengine ni ilani za vyama vya siasa zitayarishwe kwa namna ambayo hazitawagawa Watanzania kwa misingi ya dini, kabila, rangi, jinsi ama eneo analotoka na Serikali na taasisi za dini na zile za kijamii zishirikiane kuandaa mikakati endelevu ya maadili ya kitaifa

Rais Kikwete alikubali hoja zote zilizofikiwa katika mkutano huo akipendekeza kuwa katika suala la kukutana mara mbili kwa mwaka na viongozi hao, ligawanywe katika mafungu mawili.

Alisema fungu la kwanza liwe lile la kukutana na viongozi kutoka katika madhehebu na jumuiya mbalimbali kwa nyakati tofauti na lile la pili viongozi wote wa dini na serikali wakutane kwa wakati mmoja.

Hata hivyo, kama ilivyokuwa katika siku ya kwanza ya mkutano huo, wahandishi wa habari jana pia hawakuruhusiwa kuingia katika mkutano huo wakati majadiliano hayo yanaendelea.

Waziri wa Nchi Ofisi  ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge) ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa Mkutano huo, Philip Marmo alikijiuta katika wakati mgumu jana asubuhi baada ya waandishi wa habari kumbana awape maelezo endapo hawatakiwi kwenye mkutano huo.

Waandishi hao walitaka Marmo aeleze kwanini amekiuka ahadi aliyoitoa mwanzoni kuwa waandishi wa habari wangeruhusiwa kuingia katika mkutano huo na kwanini vyombo vingine viliruhusiwa na vingine kukataliwa. Chombo kilichoruhusiwa katika mkutano huo ni TBC1 pekee.

Hata hivyo, Waziri Marmo hakutaka kujibu swali hilo akieleza kuwa ana haraka, kitendo ambacho kiliwafanya waandishi wa habari wamzuie kwa nguvu na kuendelea kumhoji.

Baadaye Marmo aliwaomba waandishi hao kutulia akiwaahidi kwamba wataingia katika majadiliano, lakini pia hakutekeleza ahadi yake hiyo.

“Jana niliona hali inataka kuchafuka ndiyo sababu nikiwa kama mwenyekiti nikachukua hatua ile ya kuwafukuza. naomba mnisamehe na hao TBC1 walirusha zile habari kimakosa walitakiwa wachukue picha kwa ajili ya kumbukumbu za kiofisi tu,”.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Sunday, 16 May 2010 21:42
 

Comments 

 
0 #47 2010-05-17 11:46
Kauli za Raisi wa Tanzania sinasikitisha sana, mpaka sasa hatujui kama anapinga rushwa? Suala la upeo wake kuhusu suluhu ya matatizo ya kijamii nalo bado ni mjadala,Sijui Nchi hii ya Tanzania imekosa nini jamani. Raisi huyuhuyu amewahi kupinga mgomo wa TUCTA akijua kabisa ni maju[NENO BAYA] ya Mahakama, ni huyuhuyu aliyejitetea suala ya mafisadi tunaiachia mahakama ifanye kazi yake kwa uhuru, ni huyuhuyu aliyenukuliwa akidai ana majina ya watu wanaohujumu bandari, na ni huyu pia aliyetoa tangazo kwa wezi wa taifa ili warudishe fedha walizoiba Bot, na ni huyu aliyedai mafidadi wana nguvu sana. Na sasa ni huyu anayedai takrima haikwepeki huku akijua mahakama ilishabatilisha na hivyo serikali inatakiwa kutekeleza. Sijui watanzania wenzangu mnahitaji taarifa gani ili kufanya maamuzi sahihi juu ya CCM.
Quote
 
 
0 #46 2010-05-16 18:50
Kumtaka Kikwete achukie au kuondoa takrima wakati ndiyo ilimuwezesha kuibia benki yetu na kuwa rais ni sawa na kumwambia simba aache kula nyama. Kwa ufupi ni kwamba Kikwete ni rais wa hovyo aliyewahi kukalia kiti cha rais na kukichafua. Hafai hata kuwa balozi wa nyumba kumi zaidi ya kiranja wa starehe hasa disco. Hamuoni mkewe anavyomtumia kuchuma kama lile jambazi la kike Anna Mkapa aliyempotosha Ben akaishia kuwa kama Samson? Ila mambo hubadilika. Kuna siku Kikwete atalipia hata kama ni kwa kunyea debe.
Quote
 
 
+2 #45 2010-05-16 16:28
Unajua nchi imeharibika kila mahali, hawa viongozi wa dini ndo walisema jk chaguo la mungu sio, watu wakamchagua kwa nguvu wakijua ala kumbe hata mungu anamkubali, waapi, zengwe tu sasa tunaona namna alivyo.
Inamaana mtu ukienda hospitali ukatibiwa ukapona unatakiwa umpelekee kuku daktari ee, ukimwona kiongozi wa serikali akatatua shida yako unatakiwa umkirim sio, sasa tumekwisha miaka mitano ijayo cha moto tutakiona. Pole tanzania endelea hivyo hivyo na amani ee na utulivu ee mbivu zaja okey.
Quote
 
 
0 #44 2010-05-16 13:56
rushwa ina historia ndefu toka kpnd cha nyerere,kpnd kile kulikua na misamiat kama mnyonyaji,bwany enye n.k,maisha wazee wanasimulia yalikua magumu sana kiasi ililazim 2 kudai rushwa kwa wafanykaz,kila kitu ilikua ni folen
Quote
 
 
0 #43 2010-05-16 12:06
Sawa kweli Kilimanjaro ni kama mila na desturi pale unapozungumzia suala la kuwaita wazee na kukaa nao kuwaomba ushari lazima kuwe na kinywaji, lakini sio lazima kwa uchaguzi maana kura ni haki ya kila mtu. na si lazima utoe kitu ili upate kura. jamani hebu tubadilike.
Quote
 
 
0 #42 2010-05-16 10:59
Eh mungu wangu!si huyu huyu aleingia madarakani kwa mbwembwe mno maisha bora kwa watanzania,dah af kauli mbiu ya ari mpya,nguvu mpya na kasi mpya moja kwa moja ali2lenga vijana!basi badala ya kuwaita wale wazee wake pale diamond angewaita vijana then awaimbie mipasho yake!,wazee wa nchi hii bwana yani wamekuwa watù wa kupelekwa pelekwa tu!af 2cwalalamikie washauri wake kuwa hawamshauri,yey e ni m2 mzima bwana ana akili zake timamu,na ndo zinam2ma anatapika hovyo hovyo though yeye anaona sawa tu!nguvu mpya kweli ndg zangu mkuchika ni nguvu mpya kweli,prof kapuya je?mzee wangu makamba?kingunge?,wapo wengi sana sema ndo hivyo haina haja ya kuwalalamikia washauri wake!ni yeye mwenyewe na akili yake!kuna misemo ushauri wa mkuu ni amri!
Quote
 
 
0 #41 2010-05-16 10:53
Ndugu Mhariri wa Gazeti hili la Mwananchi. Tunaomba uhakkikishe kuwa Rais Kikwete anayasoma maoni haya. Hakikisheni mnayaprint na kumpelekea ili aweze kuona namna ambavyo watanzania wa leo sio wa kudanganywa.
Quote
 
 
-1 #40 2010-05-16 10:02
MH TUKISEMA WATU WAMESHINDWA KAZI WANAKATAA, HAYA SASA MI SIMO
Quote
 
 
0 #39 2010-05-16 07:21
Huyu jamaa kila siku ananichanganya nashindwa kuelewa kama ni mzima ama la.. inakuwaje kiongozi kuzungumza maneno yasieleweka mbele ya jamii yanayompotezea sifa kila kukicha, ni kwamba ana washauri ama?. ipo siku ataruhusu mauaji ya wagonjwa wa ngozi akisema bila viungo vyao huwez kushinda kwa tabia anayoenda nayo
Quote
 
 
0 #38 2010-05-15 22:32
rais anahalalisha rushwa! Mtuumeeeeee!
Quote
 
 
0 #37 2010-05-15 21:16
Kazi ni moja tu ndiyo waliyoajiriwa kukaa pale ikulu nayo ni kuhalalisha rushwa kuwa sehemu ya maisha yao kisu leo kimewakalia kooni wanabadilisha usemi kuwa TAKRIMA wapiii rushwa ni rushwa haiwezi kuwa takrima hawa wachaga nani kawafundisha kama siyo wao achana hizo kaka.
Quote
 
 
+1 #36 2010-05-15 20:27
Rais asiyejua hata kuchagua cha kuongea!
Quote
 
 
0 #35 2010-05-15 18:27
zao la rushwa kikwete hawezi kupambana na rushwa wakati wao wenyewe wanaishi madarakani kwa rushwa...hakuna kitu inaitwa takrima ni rushwa tu !
Quote
 
 
0 #34 2010-05-15 18:07
Wachaga wanapenda sana vitochi, hii tusikatae! Ila kuhalalisha vitumike kwa ajili ya kuombea kura hiyo sasa ni hatari kwa nchi! Ila alieubuni muundombinu huu wa kuwatumia viongozi wa dini kuhalalisha uchafu wa aina hii na viongozi hao kukubali kuingia mtegoni huyo ni Jasiri!
Quote
 
 
0 #33 2010-05-15 17:35
Mimi naungana na "Mkonombwa" na Lengai kuwa rushwa lazima CCM watatoa wakidai ni takrima.Chukueni msiogope lakini lengo letu liwe moja tu."KUITOA CCM NA JK MADARAKANI". Viva Watanzania Viva vijana,Viva Africa.Hakikisheni mnalinda kura mpaka zihesabiwe.
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner