MwanzoContactsEmail
Home Makala Siasa Uchaguzi 2010 Ahadi za wagombea urais
BOOKMARK THIS PAGE
Uchaguzi 2010 Ahadi za wagombea urais  Send to a friend
Friday, 15 October 2010 12:30

 

Ahadi za Kikwete:

1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora 

  1.  Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini
  2. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria-Igunga
  3.   Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga 
  4.  Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma
  5. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini 
  6. Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma
  7. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera
  8. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi-Kagera
  9. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba-Bukoba Mjini
  10. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  11. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera
  12. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera
  13. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu-Kagera
  14. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya
  15. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba-Kagera 
  16. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  17. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika-Mwanza 
  18. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza
  19. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita 
  20. Kulinda muungano kwa nguvu zote-Pemba 
  21. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro  
  22. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa-Mbeya mjini  
  23. Kujenga bandari Kasanga –Rukwa 
  24. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  25. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya
  26. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga  
  27. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa 
  28. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka  Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na  barabara kuu ya Moshi -Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro 
  29. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini
  30. Kuboresha barabara za Igunga -Tabora  
  31. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari  zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu 
  32. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini
  33. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)-Hydom Manyara
  34. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa- Musoma
  35. Kulinda haki za walemavu- Makete
  36. Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini
  37. Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha  
  38. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  39. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma– Kaliua,Tabora  
  40. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi-Arusha Mjini
  41. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma
  42. Kuwafidia  wanakijiji ng’ombe  waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido 45.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga 
  43. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha –Arusha mjini
  44. Kukopesha wavuvi zana za kilimo-Busekera, Wilaya ya Musoma, .
  45. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido
  46. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti –  Ngorongoro
  47. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara
  48. Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini 
  49. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa 
  50. Kuhakikisha  Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa  
  51. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania-Iringa
  52. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda
  53. kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara
  54. kuwapa wanawake nafasi zaidi-Kilolo ,Iringa
  55. ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  56. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa-Kabandamaiti  mjini Zanzibar 
  57. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti  
  58. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma
  59. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma
  60. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) –Ruvuma
  61. Ahadi Rais wa Marekani  Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma 
  62. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  63. Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara
  64. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha
  65. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa-Kibaha
  66. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha 

 Ahadi za Dk Slaa:
1.Kujenga nchi isiyo na ufisadi
2.Kufufua Tanganyika ili irejee mezani kujadili muungano na Zanzibar
3.Kufufua uchumi wa nchi kwa kutumia rasilimali zilizopo
4.Kukata asilimia 20 ya mshahara wa rais
5.Kupunguza mishahara ya wabunge kwa asilimia 15
6. Kuweka Mwenge wa Uhuru Jumba la Makumbusho
7. Kutoa huduma bora za afya bure
8. kufuta kodi ya vifaa vya ujenzi
9. Kuwalipa wazee wa EAC fedha zao ndani ya siku 100
10. Kubana matuzi Ikula (Yuko tayari kula mihogo

)

 

 Ahadi za Profesa Lipumba na Maalimu Seif:
1.Elimu ya bure kuanzia msingi hadi chuo kikuu
2.Kubana matumizi kwa kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri
3.Kuunda serikali shirikishi
4.Kusimamia rasilimali
5.Kuimarisha miundombinu
6. Kusimamia na kuboresha afya
7. Kuboresha kilimo, viwanda na uwekezaji
8. Kurudisha chakula cha bure mahospitalini

Maalimu Seif Sharif Hamad
1. Zanzibar kuwa kama Hong Kong – Unguja
2.Kuendeleza mashamba ya Karume- Kibanda maiti
3. Kubadilisha katiba na kuunda katiba mpya ya muungano na Zanzibar-  Pemba 
4.Kubadilisha mfumo wa uteuzi makamishna wa tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC)- Unguja
5. Kuwaunganisha wazanzibari ili kujenga umoja, udugu na ushirikiano-Pemba  
6. Kuwasilisha hoja ya kubadili katiba ya Zanzibar na ya Muungano-Viwanja vya Kibanda Maiti
7. Kuondoa bajeti ya ZEC isiwe chini ya waziri kiongozi na badala yake kuwa inajitegemea yenyewe- Pemba
8. Kuondoa ulazima wa mwenyekiti wa tume kuwa jaji na badala yake awe mtu anayejua sheria-Unguja 
9. Serikali kuundwa na vyama vyote vilivyopata  ridhaa ya kuchaguliwa na wananchi- Unguja
10.Kujenga jamii yenye maelewano na umoja -Pemba 
11.Kutokochagua kiongozi kwa urafiki bali kwa uwajibikaji na uadilifu -Unguja na pemba 
12.Kudhibiti vyombo vya dola vinavyofanya kazi kwa matakwa ya watu binafsi -Kibanda maiti
13.Kukomesha rushwa-Mkanyageni  Mkoa wa Kusini Pemba
14.Kuhakikisha ununuzi wa zabuni unakuwa wazi na wananchi kuruhusiwa kuhoji kuhusu zabuni-Jimbo la ole Pemba
15.Kuongeza kima cha chini cha mshahara hadi Sh150,000-Mkanyageni  Pemba 
16.Kubadili vikosi  vyote vya usalama  na kulipwa mishahara kima cha chini kulipwa Sh180,000-Chakechake Pemba
17.Kubadilisha kikosi cha KMKM kuwa kikosi cha mwambao-Wawi
18.Wazee kupanda daladala bure na wale wasiokuwa na watoto kulelewa bure-Majimbo ya Chakechake
19.Kufuta michango yote ya shule za msingi na sekondari, kila mwanafunzi kuwa na kompyuta na badala ya kuishia darasa la saba sasa kuishia kidato cha sita-Hoteli ya Bwawani
20.Kutoa kitambulisho cha kila Uzanzibari na kufuta cha Mzanzibari mkaazi- Uwanja wa Hospitali ya Mnazi Mmoja 
21.Kila mzanzibar kupata pasi ya kusafiria- Hoteli ya bwawani Zanzibar
22.Kuanzisha shirika la ndege Zanzibar -Viwanja vya Kibanda maiti
23.Kupandisha uchumi wa Zanzibar kutoka 6.8 hadi 15 kila mwaka  kwa Zanzibar -Unguja
24.Kutoa uhuru zaidi  kwa vyombo vya habari pamoja na kusaidia uanzishwaji wa Baraza la Habari Zanzibar-Unguja na Pemba
25. Kuweka hadharani nambari  yake ya simu - Viwanja vya Kibanda miti 
26. Kubadili sheria ya uwekezwaji-Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar 
27.Kila mwanafunzi kuwa na komputa yake-Viwanja vya Kibanda maiti
28.Akiwa rais hata waziri au mkewe atafungwa akiwa ametenda kosa-Viwanja vya Tibirizi Kisiwani Pemba 
29.Kujenga  bandari ya Mkokoto na Pemba ili kuweka usafiri wa haraka wa boti ziendazo kasi-Tibirizi Kisiwani Pemba
30. Ahadi kudhibiti kuvuja kwa mitihani- Unguja

Dk  Mohammed Shein 
1) Kuboresha maisha ya wavuvi-Chakechake Pemba
2) Kusomesha wafanyakazi-Mnazi mmoja
3) Kipaumbele katika elimu -Unguja na Pemba
4) Kipaumbele katika afya-Makombeni Mkoa wa Kusini Pemba.
5) Kuulinda Muungano- Wawi kisiwani Pemba
6)Kuleta mabadiliko Zanzibar-Pemba na Unguja 
7)Kuboresha Bandari ya Zanzibar kwa kuijenga upya-Kibandamaiti
8)Kuboresha Maendeleo Zanzibar- Jimbo la Wete, Pemba
9.Ujenzi wa maktaba kubwa na nzuri Kisiwani Pemba- Mtambwe
10.Kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu Zanzibar- Kijiji cha Kambini Mchangamdogo
11.Kuimarisha miundombinu Kisiwa cha Pemba- Kijiji cha Makombeni  Mkoa wa Kusini Pemba
12.Kuhamasisha wawekezaji kuwekeza  Pemba katika miradi mbalimbali-Makombeni Mkoa wa Kusini Pemba.
13.Ahadi eneo la Micheweni kuwa maeneo huru ya uchumi- Micheweni Kaskakzini Pemba
14. Kumaliza matatizo ya maji mkoani -Mkoani 
15..Kujenga Bandari ya kisasa katika eneo la Mpiga Duri Unguja- Mkoani 
16.Kuiamrisha makazi bora kwa Wazanzibar- Mkoani



Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Thursday, 21 October 2010 16:44
 

Comments 

 
0 #42 2010-11-08 11:25
NINAOMBA SERIKALI IUNDE TUME KAMILI YA UCHAGUZI AMBAYO ITAKUWA NA WATENDAJI WAKE KTK NGAZI ZA WILAYA NA MIKOA, ILI KUEPUSHA VURUGU NA KUJENGA UAMINIFU WAKATI WA UCHAGUZI.
Quote
 
 
0 #41 2010-11-08 09:58
DR Slaa usikate tamaa umewaamsha wengi baba ila walio wengi bado wapo gizani kp it up
Quote
 
 
0 #40 2010-11-06 14:10
Tusome neno la Mungu katika kitabu cha Yohana sura ya 16:33 "These things I have spoken to you, that in me (MUNGU) you may have peace. In the world you will have tribulation; but be of good cheer, I have overcome the world"
Mungu atubariki, tunaye mtetezi wetu wa haki.
J. Nyanda
Quote
 
 
0 #39 2010-11-06 14:04
Nilipendekeza kuwa uapishwaji uwe na subira!! Lakini naona umefanyika leo 6/11/2010!
MunguIbariki Tanzania kutana na viongoziwote wafungue macho waweze kusikiliza maoni ya wananchi wanaowaongoza!
Ombi langu lingine kwa mteule na wote walioko madarakani wanaoweza kutoa tamko au maamuzi ya nani awajibike wapi! Naomba na nasihi saana yafuatayo:
Majimbo yote yenye utata wa matokeo ya ubunge naomba yafanyiwe kazi hofu yangu kubwa ni kwa yule mbunge asiye na ridhaa ya wananchi atasaidiaje au atawawakilisha vipi wananchi katika jimbo lake??? mfano Segerea, Kahama , Buchosa, Tarime, Kibaha na huko Lindi!
Tusaidiane ndugu zangu na kama nisemayo hamyaamini basi Mungu hafichwi jambo kuna siku mtakuja sema kuna mtu mmoja alisema jambo hili na likapuuzwa!
Malamiko ya mgombea urais kupitia CHADEMA nayo yasitupwe yachunguzwe zaidi pamoja na Rais mteule katangazwa sio mbaya kuweka bayana ili kufuta madukuduku ya wananchi.
Ushabiki wa waandishi nao uangaliwe maana wanawezakuandik a mambo kwa kuchanganya habari na kuchanganya wananchi, mwandishi mzuri ni yule anayeandika ukweli na hata akiulizwa aweze kutoa ushahidi.
Kwa [NENO BAYA]lizia nawatakia Baraka njema matumaini yangu makubwa Mungu wetu atasimamia yote yaliyombele yetu!
Mungu Ibariki Tanzania, Bariki Bunge jipya na ahadi za kampeni zitimizwe! mteule aliahidi mambo 68 yaliyikuwa yakitangazwa na vyombo vya habari na niliyoyaona katika ukurasa huu mtukufu.
Amani ya Bwana ikae nasi sote!
J Nyanda
Quote
 
 
0 #38 2010-11-06 07:08
Mmesahau kikwete alisema atajenga barabara kwa kiwango cha lami kupitia mambali bukene mpaka Tabora, Kwa kweli tumepigwa changa la macho!
Quote
 
 
+1 #37 2010-11-05 18:03
Professa Lipumba msomi wa ukweli hotuba yako wakati wa kutangazwa mshindi imenifurahisha sana ni ya changamoto kwa tume na kwa Rais Kikwete na serikali yake hususa kwenye idadi ya kura alizopata ukilinganishwa na uchaguzi uliopita inaonyesha ni jinsi gani kuna mapungufu katika uongozi wake kama kweli wanataka kuendelea kuongoza 2015 tekelezeni ahadi zenu vinginevyo Tanzania ya leo sio ya jana'mfisadi ni tatizo linalo hitaji majibu ya ukweli sio blabla.
Quote
 
 
0 #36 2010-11-05 12:53
Watanzania, tuendelee kumwomba MUNGU KWA AJILI YA NCHI YETU!! MUNGU ALIBARIKI BUNGE NA AWAFUNIKE WABUNGE HASA WA UPINZANI AMBAO INAELEKEA CHAMA TAWALA KITAWAPOKEA KWA UNYONGE KUTOKANA NA KUWACHELEWESHEA HAKI YAO KWA KUCHELEWESHA MAJIBU NA WENGINE KUWAIBIA KURA KIAINA!! NAOMBA MUNGU PIA KIONGOZI WA BUNGENI AWE MTENDA HAKI ASEMAYE UKWELI DAIMA, MPINZANI AUNGWE MKONO NA MAONI YAKE YAFANYIWE KAZI!!
TUME YA UCHAGUZI ISIKIE KILIO CHA WAANDISHI WA HABARI ( MKUTANO WA 4/11/2010) WALIKUWA WAKIULIZA NA KUTOA USHAURI KUHUSU TUME KUTEULIWA SERIKALI NA IMETEULIWA NA CHAMA AMBACHO NACHO KIMO KWENYE MCHAKATO WA KUCHAGULIWA! NI LAZIMA KIMPENDELEE BOSI WAKE BASI NA IWE "TUME HURU" IKIWEZEKANA BUNGE LIPITISHE KAMATI AU KURUGENZI YA TUME YA UCHAGUZI.
SWALA LA DR W. SLAA LISIPUUZWE TANZANIA TUMEJALIWA AMANI SIONI SABABU YA KUKIMBILIA KUAPISHA MSHINDI WAKATI KUNA UPANDE UMELETA LALAMIKO!! NI HERI TUCHELEWESHE KUMWAPISHA MTEULE TUMALIZE TATIZO, NCHI NI YETU WANOTAWALIWA NI WANANCHI, PAKIWA HAPANA MWAFAKA ITAKUWAJE?? MTEULE UTAKUWA NA RAHA GANI YA KUTAWALA WATU WENYE DUKUDUKU?? HATA KAMA UKWELI UKIJULIKANA NA TUKACHUKUWA MWEZI AU WIKI ZAIDI KUFIKIA MWAFAKA KUNA TATIZO GANI?? AU WATASOMBWA WATU KUTOKA MIKOANI KUJA KUSHIRIKI MTEULE KUAPISHWA?? TUWEKE MAMBO SAWA ILI TUFURAHI PAMOJA! UPINZANI UPO KWA AJILI YA KUWEKA CHANGAMOTO ILI KUENDELEZA NCHI YETU KIMAENDELEO NA KUDUMISHA AMANI NA SIO KUNYANYASA NA KUWANYANYAPAA!! DAIMA TUKUMBUKE WOSIA WA BABA WA TAIFA! ASANTE MUNGU KIPINDI CHOTE CHA KAMPENI HOTUBA ZAKE ZILIKUWA ZIKIWEKWA NA WATU WAMESIKIA NA YOTE YANAYOTENDEKA NCHINI SIO MAGENI NA WATANZANIA SIKU HIZI WAMEAMKA WANAJUA MBIVU NA MBICHI PUMBA NA KILICHOBORA!! NAIPENDA SANA NCHI YANGU NI MZALENDO HALISI MWENYE UCHUNGU SAANA NIKIONA MAMBO HAYAENDI SAWA!! NATAMANI MAONI HAYA YANAYOTOLEWA KATIKA UKURASA HUU WATU WASOME NA WAHUSIKA WAJIREKEBISHE KWELI TUWE NCHI YA AMANI NA UPENDO NA USAWA!! UNAJUA UWONGO UKIWA KARIBU NA UKWELI WATU HUMEZEA LAKINI UONGO UKIZIDI HATA [NENO BAYA] ANAGUNDUA!!
MUNGU AWAFUNIKE WOTE WENYE MAPENZI MEMA NA NCHI HII, AWAFUNGUE MACHO WALE WALIOZIBWA MACHO NA KUWA HAWAONI TENA KUWA WAFANYACHO HATA MUNGU ANAKASIRIKA!!
HEBU TUSIMKASIRISHE MUNGU AKALETA GHARIKA KAMA LA SODOMA NA GOMORA!!
MMBARIKIWE,
J NYANDA
Quote
 
 
+1 #35 2010-11-04 10:31
Kwakweli matokeo ya urais sikubaliani nayo, haiwezekanai vyama vya upinzani vipate viri vingi vya wabunge na madiwani halafu mshindi atangazwe wa ccm, mfano mzuri ni Nyamagana na ilemela, kwakweli ni halali Dr Slaa akatae matokeo hayo.
Quote
 
 
-3 #34 2010-11-03 22:22
Mbona ahadi ya Dr slaa,umeziacha, Kujenga Tren ya kasi Mwanza to Dar(3hrs) ndani ya cku 1oo,Katiba mpya.Mfuko wa Cement(saruji)k uwa Tsh 5000/=,
Quote
 
 
0 #33 2010-11-03 18:03
Kuna haja ya kumtaka mtoaji maoni aweke anwani yake kama kuna nia njema ya kufanya hivyo ? Acha tu weye. ?
Quote
 
 
0 #32 2010-11-03 17:59
Kuna haja gani kutaka kujua jina na anwani ya mtoa maoni iwapo kuna haja ya kujua maoni ya wananchi. Kutaka mumjue itasaidia nini iwapo sio haja ya kumdhalilisha. Acha tu weye.
Quote
 
 
+1 #31 2010-11-03 13:46
Inakuwaje mtu anachagua chadema kwa kiti cha ubunge na udiwani halafu raisi ni CCM?
kama hawa chama cha majangili hawaja chakachua kura zetukuogopa aibu?
Quote
 
 
0 #30 2010-11-03 11:34
Kweli Nimeamini mtu usipokuwa na elimu ni rahisi kudanganyika!! na u maskini unaweza kupelekeshwa kama mzigo!! Watanzania tumesikiliza kampeni,na wagombea wamejinadi na waliokubali kuingia katika midahalo tumewasikia sera zao na ndipo tukapata mwanga nani wa kumchagua kutokana na umakini wake na jinsi gani atasaidia kero za wananchi.
Chakusikitisha, wakati wa kusubiri matokeo wengi wamekuwa makini kama tulivyokuwa tunasema "Hadi kieleweke" yaani kukaa na kusubiri matokeo baada ya kura. Mambo yamekuwa tofauti, sehemu zilizokuwa na upinzani mkali matokeo yamecheleweshwa hata kuelekea kuvuruga amani tuliyozowea TZ! Haki ya mtu daima haiibiwi mimi naomba tukubaliane na ukweli watu wanamwamko na wanataka mabadiriko na wanachagua wampendae. iweje matokeo yanakuwa tofauti!!! habari zinazotangazwa kuhusu matokeo kweli Mungu mwenyewe ajidhihirishe ukweli ujulikane!maana kuna matokeo yanayotolewa yanazidi hata idadi ya wapiga kura wa sehemu husika!! au jimbo limechukuliwa za chama cha upinzani lakini kura za urais na wabunge zinakuwa tofauti ina maana wapiga kura wampigie diwani tu na rais , mbunge awe tofauti? Kuna kituo Dar kililalamika kuwa iweje tulikubali kuwa na vyama vingi,iweje tukipenda kuwapa wapinzani inakuwa na tatizo?? Tanzania ni yetu,na tunachochaguwa ni wakutuwakilisha katika vyombo vya maamuzi na kutuwakilishia wananchi na wananchi tuwatume shida zetu mjengoni.
Mara zote mazungumzo ni mazuri kwa pande mbili zilizokaa na kuongelea maswala yao kwa umakini ili kufikia mwafaka! sasa itakuwaje kupa[NENO BAYA] kiongozi katika jimbo asiyekubalika? wananchi wataongea nae vipi ili awe mwakilishi wao?
asante Mungu Ibariki Tanzania
J. Nyanda
Quote
 
 
0 #29 2010-11-03 08:46
wametoa haadi nyingi sanaaa je watazitekeleza?.Na pesa watazitoa
wapi?.
Mie yangu macho.
Quote
 
 
0 #28 2010-11-02 12:33
nachukia watu wanafiki hasa viongozi. walijifanya wapinzani lakini baadaye eti "kura zangu zimwendee kikwete" Huo ni unafiki mkubwa kwani walikuwa wanapinga nini? ni imani gani wayojenga kwa watanzania hasa wanachama wao. tumechoshwa na watu walio maskini wa kufikiri. afadhali maskini wa mali kuliko maskini wa akili.
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner