|
Rafiki yako anapokusaliti unamchukulia hatua gani? |
Send to a friend |
|
Saturday, 28 January 2012 09:36 |
|
Herieth Makwetta KATIKA mambo ambayo huwa magumu katika kuyafanyia maamuzi, ni kwa upande wa mpenzio na rafikiyo. Hawa wote ni watu wa aina moja kwa kuwa si ndugu zako bali ni watu wako wa karibu. Lakini ni wazi kuwa upendo huzidi kwa mpenzi zaidi na si rafiki. Katika maisha ya kila siku huenda siku moja rafiki yako akatongoza au kutongozwa na mpenzi wako, naye bila hiyana akakubali je utajisikiaje pindi utakapogundua umesalitiwa baina ya hawa watu wako wa karibu? Swali la wiki lilihoji "Ukigundua kuwa mpenzi wako ana mahusiano ya kimapenzi na rafiki yako wa karibu utachukua hatua gani?" Wengi walichangia.
Fia Bright Wape nafasi kwa kuwaambia, kwanza watasikia aibu, pili lazima aibu iwafanye wajutie!
Pax Joseph Utakaa chini ujue tatizo liko wapi.
Keytone Allen Waache waendelee, maisha ni mafupi sana yafurahie..
Grace De Gregory Siwezi kusema naogopa ushahidi
Habiba Charles Dah inauma sana bora nisigundue! iwe siri yake na huyo best friend wake.
Sebastian Shirima Mimi nampiga chini tu ndilo lililobaki.
Pendo A Sanga Mimi nitamwambia jamaa kuwa hapaswi kunifanyia hivyo mimi mwanaume mwenzake kwani "ukisosombola vya wenzako na vyako watakusosombolea"
Habiba Charles Mwachie akaangaike weeee lakini jioni lazima akirudishe nyumbani.
Lissa Massala Penzi likishaisha hakuna jinsi, waache wafurahie penzi lao, lakini kuwaambia ukweli ni lazima.
Oltesh Shange Na ukiwacha huoni kama utaumia sana? Ila usilazimishe mapenzi pasipo na penzi! Moyo wangu ni mwepesi sana kukubali matokeo! Huwa naamini kama kuna mwanzo, basi na mwisho pia upo!
Gati Saimon Hata umpe nini, penzi likiisha huna jinsi!! Watu wanapewa gari, nyumba na nyama ya ulimi mpaka anatapika, lakini bado anatoa penzi kwa muuza mkaa!
Mujuni Gaulah Kajala Mapenzi siyo ya kuyachukulia kirahisi kihivyo, ndiyo maana watu tunamwagana kila siku.
Emanuel S Mrindoko ? Mbona rahisi sana katika hilo unasamehe ushaibiwa na wewe unaenda kuiba .
Janeth Mwenda Wahenga walisema 'Penzi la mama haliishi' lakini sio hayo mapenzi yenu ya kisasa, yanaisha na kusahaulika kabisa!
Gabriel Mathew Nsangaluf Jr. Ukimegewa wako nawe tafuta mnyonge ummegee.
Upupu Limitedi Inabidi hapo ujimwilike wewe kwanza unaweza kuta wewe ndio chanzo cha tatizo
Martin Jofrey G Lazima kuna mapungufu mahali! inabidi kujichunguza upya.
Halima Lameck Ni kuachana nae kwani hatakua na mapenzi ya kweli James Victory Nitashukuru sababu atakuwa amenifundisha kuwa nina mapungufu sehemu fulani pia nitawaacha waendelee.
|