
| Ukubwa pesa, ..ndevu uzee tu! | Send to a friend |
| Saturday, 28 January 2012 09:39 |
|
Hivi ushawahi kuibuka Moshi mwisho wa Mwaka? Kuna washua na midevu yao unaambiwa huwa wanawaamkia watoto wao wakirudi kutoka tauni kuzisaka, nje nje unaambiwa bila noma wala nini unakuta zee la kichagga linamwambia mwanawe, "Shikamoo mwanangu!" Sipondi kwetu lakini hizi ishu za kuchakarika kwa nini ziko kwenye baadhi ya makabila halafu kwetu kunadorora, maana ukisikia duka ujue ni kwa Mangi, makabila mengine wachaaaahe sana au kwa mpemba, ina maana sisi wazigua tumeshinfdwa kuwa na maduka? Hatuna hela au hatujui biashara? ...imenitachi sana hii na imekuja kutokana na ishu moja hivi niliisikia kitaa, ilikuwa kama sio ya ukweli hivi lakini pia inatoa fundisho ikiwekwa kwenye masomo kama haya ya kitaa. Urafiki ukajengeka nini, ..mangi akaziingiza kwa mtoto, na mtoto kwa kuwa alishaona picha kwamba bila huyu mchizi homu kitakuwa hakieleweki, ..akaingia laini, kale kamchezo kakaanza! sasa si unajua zile mambo zetu zikianza? Binti sasa ikawa akitumwa kwa Mangi anachukua hata lisaa kumaliza mambo yake na mara nyingi akawa akiulizwa, anachojibu ni kwamba Mangi alikataa na alikuwa katika hatua za kumsomesha ili aelewe. Dingi akiambiwa hivyo tu unaambiwa ana'kulu dauni'. Inambidi achune tu, lakini moyoni anaumia binti kaharibiwa maisha, shule ndio ikawa basi tena, na mangi ndio humuelezi kitu. We umepata picha gani hapa? Kama mshua angekuwa mtu wa kuchakarika unafikiri angekosa nguvu ya kumvaa Mzee Mangi? Lazima angeenda kumzingua lakini kwa sababu alikuwa mtu wa kuskilizia acha ya mkute na binti ndio alikuwa jembe homu inabidi akalime kahawa moshi na mshua aendelee tu kukopa kwa Mangi na ipo siku ujue mangi atachoka, atakodi fremu mbali na pale atasepa! Acheni kufuga ndevu wanangu mwaka ndio huu, tutafuteni mkwanja sawa? |














