
| Big Brother kama Amazing Race | Send to a friend |
| Saturday, 28 January 2012 09:40 |
|
WAKATI watu wakidhani kuwa wamelizoea shindano la Big Brother Afrika, ukweli ni kwamba halitazoeleka kutokana na kuwa na ‘twist’ mpya kila uchwao. Kwa miaka sita shindano limefanyika na Tanzania imetuma washiriki mara zote, vivyo hivyo nchi nyingine, lakini sasa hakutakuwa na mshiriki mmoja mmoja bali itakuwa wawili kama shindano la Amazing Race. Mwaka huu hakutakuwa na utaratibu wa mshiriki mmoja mmoja, kila anayetaka kushiriki mwaka huu ni lazima atafute patna, yaani mshiriki lazima awe na mwenzake anayemfahamu vilivyo, kama mama, baba, kaka, mpenzi, rafiki n.k. Aidha kila mshiriki anashauriwa kuwa makini wakati wa kuchagua mtu anayetaka kwenda naye kwa kuwa ni safari ngumu ambayo itakuwa na milima na mabonde mengi. Mwaka huu zawadi imeongezeka kwani mshindi atajinyakulia kitita cha dola za Marekani milioni 300 kamili. Nchi ya Ethiopia haitashiriki mwaka huu, mwaka juzi iliwakilishwa na Yacub, mwaka jana, Hanni. Hata hivyo nchi za Liberia na Sierra Leone zitashiriki kwa mara ya kwanza. Fomu za ushiriki zitaanza kupatikana mtandaoni kuanzia februari 5 mwaka huu na mwisho wa kuzijaza ni februari 27. |














