MwanzoContactsEmail
Home Makala Starehe Kili Awards 2012, iwe bora zaidi...
BOOKMARK THIS PAGE
Kili Awards 2012, iwe bora zaidi...  Send to a friend
Saturday, 28 January 2012 09:41

Miguno baada ya kichwa cha habari najua itakuwepo, kwanza kwa wapinzani pili kwa waandaaji lakini hilo si la kujali sana iwapo kuna ufafanuzi wa kile nilichokitanguliza, hili nililoandika ni msisitizo ili wadau wasijisahau, hiki kitu ni muhimu sana kwa wanamuziki wa nyumbani.

Hakuna jambo jema kama kufanya kazi yako nzuri na ikatambulika, hili ni jambo ambalo hutoa motisha sana na kusababisha mwisho wa siku, kazi nyingi nzuri kufanyika na tasnia ya muziki kuwa kubwa na yenye ubora, mnanisikia wadau.

Sasa siku za karibuni tumekuwa tukiambiana kuhusiana na kuziboresha hizi tunzo, tangu mwaka ambao lile kundi la wadau wa muziki, lililopachikwa jina la Academy kuingia katika mchakato wa uchaguzi wa wanaostahili kutunzwa.
Huu ni mwaka wa tatu na kila mwaka tumekuwa tukiimbiana kuhusiana na kuboresha mambo madogo madogo ambayo yamekuwa kama yakitia doa, hizi tunzo ambazo zimesimama kitaifa zaidi.

BASATA wanahusika humu kwa kiasi kikubwa kama waratibu huku TBL wakisaidia kudhamini kwa asilimia mia moja shughuli ya kutunza wanamuziki.

Mwaka huu bila shaka minong'ono itapungua na kazi itafanikiwa kwa kiasi kikubwa na sisi kama wadau wa starehe twawatakia kila la kheri, wadhamini na waratibu huku tukiwakumbusha kuhusiana na wadau mtakaoshirikiana nao, wasiwe wengi kutoka sehemu moja angalieni kila eneo lipate mtu wake.Kila la kheri katika maendeleo ya sanaa ya muziki.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner