MwanzoContactsEmail
Home Makala Starehe Umeme wamuathiri Hussein Machozi
BOOKMARK THIS PAGE
Umeme wamuathiri Hussein Machozi  Send to a friend
Saturday, 28 January 2012 09:41

Kalunde Jamal
MSANII wa muziki wa kizazi kipya Huseini Machozi amelalamikia kupanda kwa gharama za kurekodi,huku akihofia kuwa kutawakimbiza wasanii wachanga.

Alisema gharama kwa sasa zimekuwa kubwa licha ya kuwepo kwa studio nyingi,kitu ambacho kinaweza kukatisha ndoto za wasanii wengi wachanga.

Machozi ambaye yupo kwenye maandalizi ya video ya  wimbo wa 'jela' alifafanuwa kuwa kama wao ambao wapo kwenye gemu muda mrefu inawapa shida itakuwaje kwa wale ambao wanajichanga ili waweze kuingia studio.

"Kwa kweli gharama ni kubwa ukitofautisha na mwezi mmoja uliopita,ingawa pia inategemea unafanyia kwenye studio gani lakini kote bei imepanda"alisema Machozi na kuongeza kuwa....

"Hii inatokana na kupanda kwa gharama za umeme na kubadilika kwa bei za mafuta mara kwa mara kitu kinachowafanya waendeshaji kupandisha gharama ili waweze kupata faida"alisema Machozi.

Machozi aliiomba Serikali kuangalia kwa undani na kutafuta jinsi ya kudhibiti mfumuko wa bei ili kuwapa unafuu wa maisha wananchi hasa wa hali ya chini.

Akionyesha kuguswa na suala hilo Machozi alisema kuwa kwenye tangazo la kupandisha bei za umeme Tanesco walisema kuwa haimuhusu mtumiaji wa kawaida kitu ambacho sio kweli.

A lisema kwa maisha ya kawaida hakuna Mtanzania anayetumia unit 50 kwa mwezi karibu wote wanatumia zaidi ya hapo na kama hutumii wewe muuza bidhaa inamgusa kwa maana hiyo atakuuzia vitu bei juu na utakuwa umehusika moja kwa moja.

Alifafanuwa huwezi kusema mtu wa hali ya chini haumuhusu,kupanda huko kunawahusu wenye viwanda ni kujidanganya na kuwafanya Watanzania hawana uwezo wa kufikiri.

"Umeshasema inawahusu wenye viwanda sio Watanzania wenye hali ya chini kwa maana hiyo si lazima waende kwa enye viwanda kununua sasa mwenye kiwanda atakubali kuuza kwa bei ya hasara kwa hiyo moja kwa moja imemuhusu mwenye hali ya chini moja kwa moja "alisema na kuongeza

"Kibaya zaidi  inamuumiza  kwani wenye bidhaa wanajua lazima utakwenda kununua au kuhitaji huduma hivyo watatoa au kuuza kwa gharama wnayotaka wao kwa kisingizio hicho hicho cha kupanda kwa gharama za umeme"alisema Machozi.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner