MwanzoContactsEmail
Home Makala Starehe Usiku wa Min ZIFF Red Carpet ulivyofana jijini
BOOKMARK THIS PAGE
Usiku wa Min ZIFF Red Carpet ulivyofana jijini  Send to a friend
Saturday, 28 January 2012 09:44

Na Michael Matemanga
WASANII na  wadau mbalimbali wa tasnia ya Filamu Nchini,mwishoni mwa wiki walikutana kwenye tamasha dogo la Filamu la  Min ZIFF Red Carpet, liliyofanyika  New Maisha Club mwishoni mwa wikiendi jijini Dar es Salaam.

Tamasha lilianza majira ya Saa 4:45 usiku kwa wasanii mbalimbali wa tasnia ya filamu Nchini,kupiga picha na kufanya mahojiano na waandishi mbalimbali waliokuwepo kwenye eneo la Red Carpet,kuingia ukumbini kwa ajili ya ugawaji wa  tuzo kwa wasanii.

Mashabiki  mbalimbali waliojitokeza kwa wingi New Maisha Club,waliweza kushuhudia wasanii wakubwa wa tasnia ya filamu Nchini wakiibuka kidedea kwenye uchukuaji wa tuzo hizo,ambazo zilianza kutolewa saa 7:30 usiku.
Tuzo zilizokuwa zikiwaniwa ni Msanii bora wa filamu,Filamu bora,Kampuni bora ya usambazaji wa filamu Nchini,Mwogozaji Bora wa Filamu pamoja na Filamu yenye Sauti Bora.

Kwenye utoaji wa tuzo hizo,wadau wa filamu za bongo waliweza kumshuhudia msanii maarufu Steven  Kanumba,akiibuka kidedea baada ya kujinyakulia tuzo mbili kwa mpigo,kwa kutangazwa kuwa ndiye  msanii bora wa filamu Nchini pamoja na filamu yake ya ‘Devil Kingdom’ kuibuka kidedea kwa upande wa Filamu yenye Sauti Bora.

Akizungumza na gazeti la Mwananchi  baada ya kukabiziwa tuzo zake,Steven Kanumba hakusita kutoa shukrani zake kwa waandaaji wa tuzo hizo pamoja na mashabiki wa filamu za bongo waliompigia kura.

Vilevile amewataka wasanii wa filamu Nchini wawe na umoja na kuwa na tabia ya kupendana,na  kudai kuwa kama wasanii wenyewe kwa wenyewe hawapendani katika tasnia ya filamu ni kazi bure.

“Nawaomba wasanii wenzangu tuwe na umoja pamoja na upendo,lakini hata tukiwa na umoja kama wasanii hatupendani wenyewe kwa wenyewe,katika tasnia ya filamu Nchini itakuwa ni kazi bule”alisema Steven Kanumba

Steven Kanumba alimalizia kwa kuwaomba mashabiki wa wa filamu za Tanzania wawe wananunua kazi za wasanii wa ndani,ambazo zinauzwa kihalali kama njia mojawapo ya kuwaunga mkono wasanii wa Tanzania.

Wasanii wengine waliojizolea tuzo hizo ni JB ambaye filamu yake ya ‘Senior Bachelor’ iliibuka filamu bora,Issa Musa(Cloud) alijinyakulia tuzo ya mwongozaji bora wa filamu,wakati tuzo ya msambazaji bora wa filamu za Tanzania ilikwenda kwa kampuni ya Sterps Entertainment.

Baada ya kumalizika kwa utoaji wa tuzo hizo msanii wa kizazi kipya wa muziki wa Bongo Fleva,AT  alipanda kwenye steji na kutoa burudani kwa mashabiki waliojitokeza kwa wingi  siku iyo,kabla ya kikundi cha Offside Trick kufunga pazia la tamasha hilo.

 

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner