
| Ni aibu kwa wanafunzi wa Tanzania kufeli kiswahili | Send to a friend |
| Friday, 23 December 2011 09:28 |
|
HIVI karibuni tumesikia kuwa ufaulu katika somo la Kiswahili kwa matokeo ya darasa la saba mwaka huu, umeshuka ukilinganisha na ufaulu wa somo Kiingereza. Waswahili husema “mdhaarau mwiba mguu huota tende, hayo ndiyo tunayoyaona sasa katika kiwango cha ufaulu katika somo la Kiswahili. Lakini katika ngazi ya elimu ya msingi na shule za upili Kiswahili hutumika, ili kukidhi mahitaji ya mwanafunzi katika kumjenga ili kuwa na msingi mzuri katika kufahamu vyema lugha yake. Tukiwa tunatafakari katika matokeo hayo, yapo mambo kadhaa yanayopaswa kutazamwa na kuchukuliwa hatua ili kuepuka fedheha kwa wanafunzi kufeli somo hilo. Hata hivyo usemi huo unaweza ukawa na athari chanya iwapo watu watachukua hatua kukabiliana na changamoto hiyo kwa kubaini ugumu kwake uko wapi na kushirikiana na wenzake katika kupitia mada zinazomsumbua ama asizozielewa vyema kwa msaada zaidi, ikiwa ni pamoja na kupitia maandiko mbalimbali ya wataalamu wa Kiswahili ndani na nje ya Tanzania. Vilevile wanafunzi wa shule za msingi wanapaswa kazingatia masomo na kwa kupunguza michezo na soga pamoja na mambo yasiyo na tija pamoja na kutafuta muda wa ziada kujisomea kwa bidii ili kuyatafutia ufumbuzi yale ambayo hayakueleweka vyema wakati wa vipindi vya darasani. Upande wa walimu wanapaswa kuendelea kufundisha somo la Kiswahili kitaaluma zaidi kuliko kufundisha kwa mazoea na kurahisisha mbinu za kufundishia kwa wanafunzi hao. Hii ni kutokana na mambo mengi yanayoelezwa katika lugha hiyo yanahusu mazingira yaliyo karibu na mwanafunzi. Hata hadithi zinazoelezewa na watunzi wa vitabu ni kutoka mazingira hayo ambapo makabila ya Watanzania ni wazungumzaji wakubwa wa lugha ya Kiswahili. Kwa hali hiyo ningetegemea kuona somo la Kiswahili linakuwa la kwanza katika ufaulu wa masomo mengine licha ya kuwa masomo mengine nayo yanafundishwa kwa lugha ya Kiswahili kwa ngazi zote kinakofundishwa. Kuwa na walimu wenye uzalendo na waliopikwa katika kufundisha somo la Kiswahili hilo, watumike ipasavyo katika maeneo yenye uhaba na si mwalimu yeyote anayezungumza lugha hiyo apewe nafasi ya kufundisha Kiswahili. Hilo linaweza kuwa na tija katika kuleta maendeleo ya kuinua kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari. Jambo lingine la kuzingatia ni kuimarisha kwa kiwango cha zana za kufundishia. Huku baadhi ya walimu wamekuwa hawazingatii hilo kwa wa kwa kuona kuwa ni kupoteza muda na gharama, wakati hata zipo njia mbalimbali za kuunda zana hizo bila gharama yeyote. Aidha katika kukabiliana na changamoto hiyo ya kuendelea kushuka kwa kiwango cha Kiswahili, pia walimu wa Kiswahili kwa umoja wao wanapaswa kuliangalia katika umoja wao walimu wa Kiswahili kwa ngazi mbalimbali. Njia pekee ni kuwa na mipango endelevu inayoakisi maendeleo ya Kiswahili katika kukikuza na kukieneza. |















Comments