
| Kulikoni Serikali inapata hasara Sh300bilioni kwa uchakachauji, wahusika wanaachwa? | Send to a friend |
| Thursday, 02 September 2010 14:17 |
|
Hasara ya fedha hizo ni kwa mwaka wa fedha 2009/2010 pekee. Uchakachuaji ni uchanganyaji wa mafuta ya dieseli au petroli pamoja na mafuta ya taa. Lengo la watu wanaochanganya mafuta hayo ni kutaka kupata faida kubwa zaidi licha ya kwamba mchanganyiko huo unaharibu mitambo ya aina mbalimbali ikiwemo ya magari, pikipiki, mashine za kusaga, mashine za kuvuta maji na mingine mingi. Wafanyabiashara hao wanachanganya mafuta ya petroli na mafuta ya taa kwa sababu bei ya mafuta ya taa ni Sh1,000 kwa lita wakati mafuta ya Dieseli au Petroli ni zaidi ya Sh1,600, hivyo akichanganya mafuta hayo anaona atafaidika. Uchakachuaji huo unadaiwa kushamiri kwenye vituo vingi vya mafuta ambavyo vingi vimejengewa ukuta ili kuficha mambo yanayofanyika ndani. Vituo vipo kuanzia Dar es Salaam hadi Mbeya, hadi Arusha, hadi Mwanza na hadi Mtwara ama Songea. Athari za uchakachuaji mafuta zimefika hadi Ikulu ambako magari ya Rais yalionja adha kule Kilimanjaro katika mji wa Moshi ambako yalizimika muda mfupi baada ya kuwekezwa mafuta ambayo yalidaiwa kuchakachuliwa. Lakini ukweli ni ni kwamba mkuu huyo wa mkoa alitoa takwimu hizo akinukuu hotuba ya Waziri wa Nishati na Madini Walliam Ngeleja aliyoitoa kwenye kikao cha Bunge la Bajeti Julai mwaka huu. Mwanajeshi huyo aliongeza kwamba uchakachuaji ni mchezo mchafu, ni kuhujumu uchumi wa Taifa, lakini akaliachia kazi Baraza husika kukabiliana na vitendo hivyo. Hoja ya msingi ni je Baraza kama hilo ndilo linatakiwa kupambana na wahujumu uchumi? Je kwa kitendo cha serikali kukwepa majukumu yake , biashara ya uchakachuaji ni ya serikali ama wafanyabiashara? Inakuwaje Rais aonje joto la jiwe kwa uchakachuaji , lakini wasikamatwe wafanyabiashara husika wote kwa kuhojiwa?. Ni kwa vipi Serikali ipate takwimu za hasara ya Sh300 bilioni, lakini wanaosababisha hasara wasikamatwe ? Lakini pia kwa jinsi serikali inavyotunza kumbukum bu za madeni kwa waliopoteza fedha za umma ama kutumia vibaya ni vigumu kuamini sababu za kujua takwimu bila ya kuwatia ndani wahusika. Bila Shaka Dk Balele alirudia kutaja takwimu za hasara kwa taifa ya Sh300 bilioni huku akiuma kidole kwamba kama angepewa nafasi ya kuwasaka angeanzia na wenye magari 18 ya Tanzania ambayo yalikutwa na mafuta yaliyochakachuliwa nchini Rwanda. Hivi karibuni tumeshuhudia magari takribani 18 yakirejeshwa kutoka nchini Rwanda kwa sababu yalibainika kubeba petroli iliyochakachuliwa kutoka Tanzania. Ni fedheha kwa serikali kuvielekeza vyomboi vingine vichukue hatua wakati watu wanaliangamiza Taifa. Serikali ikikaa kimpya dhidi ya wachakachuaji na wezi wa fedha za miradi kwa ujumla kutawafanya Watanzania wawe na imani kwamba wahusika wakuu ni vigogo wa serikali yenyewe. |












