
| Kiswahili kinaathiriwa na lugha zetu za asili | Send to a friend |
| Thursday, 02 September 2010 14:21 |
|
Napenda kuwashukuru sana baadhi ya wasomaji wangu walioniletea ujumbe kwa njia ya simu za kiganjani kuhusu maoni kwa makala ninazoandika. Maoni na mapendekezo walioniletea yamezingatiwa na yatasaidia sana katika kuboresha makala nyingine siku za mbele kwani itanibidi kuwasambazia wasomaji wengine maoni haya ili nao wafaidike. Kwa wale wakereketwa wa Kiswahili wanaojali matumizi fasaha ya lugha ya Kiswahili, nawaomba waendelee na juhudi zao na pia kujitahidi kuwaelekeza watumiaji wabaya wa Kiswahili popote wanapokuwa kwani haya ni mapambano makubwa. Iko siku ambapo wale wanaopiga vita ukuzaji na uendelezaji wa Kiswahili sanifu watasalimu amri na watatuunga mkono. Kwa hiyo katika jitihada za kuendeleza mapambano hayo, nitaendelea kuyachunguza magazeti ya Kiswahili na kukosoa pale ambapo panahitajika kukosolewa kama ifuatavyo: Mwandishi alikuwa na nia njema ya kueleza jinsi watajiri wanavyotumia suala la mpira kwa malengo yao binafsi. Lakini hakuwa mwangalifu katika mpangilio sahihi wa maneno katika lugha. Alitakiwa kuandika, “ Jambo la msingi ni kuwa matajiri wanatakiwa kuacha kutumia soka kwa kukuza majina yao na biashara zao.” Neno kimsingi mwanzoni mwa sentensi halina maana. “ Unaweza kuwafananisha na wanajeshi wanaotumwa vitani kuikomboa nchi isivamiwe na adui.” Maana ya kukomboa pia kigomboa ni kumfanya mtu aliyekuwa amefungwa au aliye katika unyonge, udhalimu au kutawaliwa awe huru. Mwandishi alikuwa na maana ulinzi wa nchi. Kwa hiyo isomeke, “Unaweza kuwafananisha na wanajeshi wanaotumwa vitani kuilinda nchi yao isivamiwe na adui.” “ Tutaendelea kufanya hivyo kwani hiyo ndiyo njia pekee ya kuinua vibaji michezo hao nchini.” Yako baadhi ya makabila hawana fonimu /b/ badala yake hutumia /p/. Tunatakiwa kujirekebisha katika tatizo hili. Pili ni matumizi ya maneno ya mwisho hayaeleweki vizuri. Maneno hayo ni ‘kuinua vipaji michezo hao nchini.’ Ilitakiwa iwe ‘ kuinua vipaji vya wanamichezo hao nchini.’ “ CCM Mkoa wa Arusha kimefanya vikao kadhaa vya siri na sasa iko mbioni kuunda kamati katika kila kata kwa mantiki ya kuondoa vitendo vya rushwa wakati wa uchaguzi.” Maana ya neno mantiki imepotoshwa na halina maana hapa. Maana ya mantiki ni mtiririko wa fikra zilizopangwa ili kujenga hoja yenye kukubalika. Haiwezekani kusema ‘kwa mantiki ya kuondoa vitendo vya rushwa.” Inatakiwa kuandika ‘kwa lengo la au kwa madhumuni ya ‘ Kwa hiyo isomeke CCM Mkoa wa Arusha kimefanya vikao kadhaa vya siri na sasa iko mbioni kuunda kamati katika kila kata kwa lengo/madhumuni ya kuondoa vitendo vya rushwa wakati wa uchaguzi. ” “ Wakati wa kampeni, mgombea anakuwa na uwezo wa kujenga visima, mashule, mahospitali na kugawa pesa huku akizunguka majimboni kwa kugawa pesa na misururu ya magari ya kukodi.” Kwa kawaida hatuongezi kiambishi ‘ma’ mbele ya maneno haya wakati wa kuandika wingi wake.
Haya ni mawazo kutoka katika lugha za kigeni. Sahihi ni kusema, ‘ jitihada zinapaswa kufanywa.’ Hivyo iandikwe, “ Ni wazi jitihada zinapaswa kufanywa katika kuhakikisha kuwa wakulima wanapata misaada ya uhakika.” Abadallah na Mango. Ambao wote kwa pamoja walikuja na mavazi mbalimbali ya ubunifu.” “ Shoo hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Serena mjini Zanzibar iliwashirikisha wabunifu wengine wawili ambao ni Farouq Abdallah na Mango ambao wote kwa pamoja walikuja na mavazi mbalimbali ya ubunifu.” Ili kuiweka sentensi hii kwa usahihi wake ilibidi kuongeza maneno machache kama ifutavyo: Ingefaa kuongeza neno ‘ ni ’ na kusomeka ‘ ni jambo ambalo linatishia…’ Pia neno ‘kiwango’ liongezwe ili isomeke ‘kiwango cha taaluma’. Kwa hiyo sentensi isomeke, |













