
| Biashara ya Kununua/Kuuza nje ya nchi | Send to a friend |
| Thursday, 02 February 2012 08:34 |
|
Elewa soko lako Na Staphord Kwanama HAKIKISHA muda wote unapata taarifa za kutosha. Jisomee mambo mbalimbali ili upate uelewa mpana wa biashara ya kimataifa. Soma machapisho ya kibiashara, magazeti ya kimataifa, na taarifa mbalimbali za fedha. Jua nani anauza nini na wapi, ingawaje biashara ya kimataifa ina wajasiriamali wengi sana lakini jitahidi kuwafahamu baadhi iwezekanavyo na namna gani wanavyofanya biashara. Unawezakuwa na bidhaa bora na zenye viwango lakini usijue utauza wapi, unapotafuta soko hakikisha unatafuta sehemu yenye mahitaji ambapo utauza kwa bei nzuri na kukufanya uendelee kustawi katika soko. Kupata soko mahususi ni muhimu sana inakurahisishia mauzo. Mara nyingi unaweza kudhani kuwa biashara ya kimataifa ni ngumu lakini ukishaanza inakuwa nyepesi na yenye maslahi zaidi kwani kuna wajasiriamali wachache (20%) wanaofanya biashara hii ukilinganisha na biashara zote ulimwenguni. Hii inakupa fursa na wigo mpana kustawi kibiashara. Itumie benki yako Unapokuwa na malengo ya kufanya biashara ya nje chagua benki inayojihusisha na biashara za kimataifa, ambapo utaweza kutuma na kupokea fedha ili kurahisisha malipo. Benki itakusaidia kufuatilia na kuhakikisha malipo yanafanywa ipasavyo, na pia inakuwa rahisi kupata uwezeshwaji kifedha kwa njia ya mkopo. Matumizi ya benki katika biashara ya kimataifa ni lazima, hivyo chagua benki bora. Makubaliano kibiashara Kibiashara, makubaliano ni moja ya mambo muhimu sana, yawezakuwa makubaliano kwa njia ya mdomo au kimaandishi, katika hali zote umakini wa hali ya juu unatakiwa ili usitoe ahadi zaidi ya uwezo wako na ukashindwa kutimiza au kuingia makubaliano ambayo baadae inakuwa hasara kwako. Kwa mfano; ukiamua kuwa wakala kuuza bidhaa za nje ndani ya nchi, inashauriwa kuwa na mkataba unaobana kisheria (sheria za biashara za kimataifa). Aidha, unapoamua kuingia kwenye ujasiriamali hakikisha unakuwa na mahusiano mazuri na watu wengi wa kada mbalimbali kama wanasheria, wahasibu, benki, washauri wa biashara, watalaam wa rasiliamali watu n.k. Mfano katika mikataba utahitaji mwanasheria ambaye anaweza kusoma na kuelewa makubaliano ndani ya mkataba na kukushauri ipasavyo. Kimsingi, unapoingia mkataba wa kuwa wakala kuuza bidhaa za nje nchini inakuwa ni makubaliano baina yako na mzalishaji, ambapo utasambaza au kuuza bidhaa katika maeneo au nchi mnazokubaliana. Mzalishaji atakulipa kamisheni mtakayokubaliana tofauti na bei ya bidhaa zenyewe, pia mzalishaji atakupa sampuli za bidhaa na kukuwezesha katika matangazo ya bidhaa husika. Kwa wewe msambazaji utahakikisha unafanya kila linalowezekana kusambaza bidhaa kadilri ya makubaliano. Mkataba pia utaelezea vigezo na masharti mbalimbali kuzingatia ikiwa pamoja na muda wa uwakala huo, kuacha uwakala kwa pande zote, n.k. Katika maongezi na wajasiriamali-mawakala wa bidhaa za nje nchini, iligundulika kuwa changamoto kubwa ni katika mikataba, wapo ambao hufanya uwakala hata bila mikataba kitu ambacho ni hatari sana kwani unaweza kuachwa solemba wakati umewekeza fedha zako pia katika miundombinu mbalimbali, hali kadhalika huwezi kuongeza uwezo kifedha kupitia benki kama huna mikataba. Na pia wengine wanayo mikataba lakini kutokana na hali duni walisaini bila kuelewa vigezo na masharti hivyo huishia kunyonywa tu. Usiharakie tu kwa kuwa umesikia kuna fursa hiyo ya kuwa wakala bali tulia na chukua muda kuelewa makubaliano ikiwa ni pamoja na mahitaji ya kisheria ya nchi. Mfano, mwaka jana nilishuhudia wakala wa bidhaa za majenerata toka nje ya nchi yakichomwa moto na kupondwa pondwa na greda kutokana na kutokidhi viwango kwa mujibu wa sheria za Tanzania, hasara ilikuwa kwa wakala husika kutokana na mkataba. Usafirishaji bidhaa Katika biashara ya kimataifa, suala la usafirishiaji (shipment) lazima mjasiriamali alifahamu vizuri gharama, muda wa kusafirisha, aina ya usafiri, mahitaji ya kisheria, namna kufungasha, ubora, mambo ya kodi na tozo mbalimbali, namna ya kupokea bidhaa, vibali na nyaraka. Katika usafirishaji kuna nyaraka hutolewa inayoitwa ‘bill of lading’ ambayo ni kama stakabadhi ya kutumwa na kupokea bidha, husainiwa na wakala wa meli kwa usafiri wa majini inayothibitisha bidhaa zimepakiwa katika bandari fulani jina la meli, muda, aina na kiasi cha bidhaa na bandari zitakaposhushwa. Katika usafirishaji kuna gharama mbalimbali kulingana na namna ulivyochagua bidhaa zako zisafirishwe mathalani kuna gharama za usafiri wenyewe, bima, kupakia na kupakua mzigo, kuhifadhi bandarini. Itaendelea…….. Kwanama ni Mkurugenzi Mtendaji Plus Finance na Mtaalam Mshauri wa mchanganuo wa biashara 0712 066 064 This e-mail address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it |














