MwanzoContactsEmail
Home Makala Siasa Wanaohitaji nyongeza ya posho ni walalahoi
BOOKMARK THIS PAGE
Wanaohitaji nyongeza ya posho ni walalahoi  Send to a friend
Wednesday, 18 January 2012 09:55

Na Mwandishi Wetu
HIVI karibuni, ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungani wa Tanzania ilipandisha posho za wabunge kwa asilimia 154 ikiwa ni kutoka shilingi 70,000 za awali hadi kufikia shilingi 200,000.
Maelezo ya Spika wa Anne Makinda ni kuwa kiwango kimepandishwa kutokana na ugumu wa maisha mjini Dodoma na pesa hizo zimeanza kulipwa toka baada ya kikao cha Novemba mwaka jana 2011.
Kauli hiyo inakinzana na ya Katibu wa Bunge, Thomas Kashilillah ambaye ni katibu wa bunge, ambaye anakaririwa akisema kuwa hakuna kitu kama hicho.
Hatua hiyo ya ofisi ya Spika Makinda ina akisi rejea ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere katika Kitabu chake TANU na UHURU.

Katika moja ya kurasa za kitabu hicho, Baba wa Taifa anauliza "Tunamwomba kila mwananchi kufanyakazi kwa bidii ili kuondoa umaskini wa nani? .
Anaendelea, Umaskini wa viongozi wa TANU? Au wa watumishi wa serikali? Au watu wachache wenye elimu, au nguvu, au bahati au ujanja?
Au shabaha yetu ni kuondoa umaskini wa kila mtu kama vile shabaha yetu ya kwanza ilikuwa kuleta uhuru na heshima kwa kila mtu?.  Mwalimu anawasaili aliowapa dhamana kisha anafumba.

Ndio maana watu fulani walipoonyesha kwa vitendo vyao kwamba kwamba hawaelewi kuwa uhuru wetu, na heshima inayotokana na uhuru huo, ni kwa raia wote, bila ubaguzi basi serikali ya TANU ilichukua hatua za kuwaondoa mashaka kabisa watu hao.
Hafafanui kuwaondoa mashaka kulikuwa kwa namna gani lakini ni wazi kuwa watu waliojiongezea na wale ambao wanaunga mkono ongezeko hilo ni wale ambao wanapingana na kauli hiyo au kwa lugha nyingine wana mashaka na uhuru wetu.

Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utohu anasema kulingana na katiba ya nchi ya mwaka 1977 kuna utaratibu wa kutumia pesa za umma.
Kwa kuwa nami nimesoma katika magazeti na kwa kuwa kuna utaratibu, katika posho hizi sina uhakika kama zipo na zimeanza kulipwa na kama zimeanza kulipwa ni kwa idhini ya nani? anahoji.
Utoh anasema ofisi yake imemuagiza mkaguzi wake wa ndani katika ofisi ya bunge kulifanyiakazi na ukweli kuhusiana na suala hilo utabainika katika ripoti ya mkaguzi ambayo inatarajiwa kutoka Aprili mwaka huu.

Anasema ni ofisi yake ndio ambayo inaidhinisha matumizi ya fedha za serikali lakini hilo limefanyika bila wao kuwa na taarifa basi ni makosa yamefanyika lakini hawezi kulizungumzia kwa undani kwa sasa.
Ofisi yangu ilipaswa kufahamishwa hivyo ofisi yangu inalifanyiakazi ili kupata ukweli wa mambo na kujua hatua za kuchukua anasema
Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema anakiri kuwapo kwa ongezeko hilo, hatua ambayo anasema kuwa linawasaidia wabunge ambao wanakabiliwa na majukumu mengi huku baadhi yao wakiwa hawana shughuli tofauti na siasa.

Mimi nafikiri hakuna tatizo, kuna watu kweli pesa hizo tunazihitaji na hata tunazolipwa hazitoshi lakini kuna ambao si waadilifu maofisini kwao, anasema.
Anasema mbunge huyo wa Vunjo kuwa kuna ambao ni mafisadi, wengine ni wafanyabiashara na pia wapo ambao wakipita makanisani wanachukua pesa.
Anakiri wananchi walio wengi vipato vyao ni vya chini na wengine wanaishi hadi zaidi ya chini ya dola moja lakini pesa hizo wanazitumia katika misaada ya hisani na pia kuchangia huduma tofauti za jamii.

Nimetumia karibu Sh 7 milioni kuchangia makanisa na huduma zingine na hizo ni pesa za posho zangu unafikiri katika hali hiyo tutafanyaje? anahoji.
Baadhi ya walimu wanadai kuwa kinachofanywa na wawakilishi hao wa wananchi ni wazi kuwa wamejifikiria zaidi wao wenyewe kuliko wananchi ambao wamewachagua.
Fikiria juu ya tofauti hiyo ya kipato ambayo inatetewa na baadhi ya wabunge anasema Mwalimu Rose Joseph wa

Chuo cha Ualimu Chang'ombe.
Anasema serikali inakabiliwa na changamoto nyingi kuanzia mikopo ya wanafunzi, umaskini wa kipato ngazi ya familia na sasa wigo mpana ambao unatengenezwa baina yao wanasiasa na wananchi wa kawaida.
Mwalimu huyo anapingana na kauli ya Mbunge Mrema na kudai kuwa suala la michango ya makanisa na huduma zingine si la mmoja wote wanachangia hata wale ambao sera zinawataja kuwa watahudumiwa bure.

Nenda hospitalini kamtafute mzee anayepata huduma bure za afya, watoto hadi kinamama wajawazito wananunua kila kitu, achilia mbali bakshishi anayodai mhudumu wa afya," anasema.
Kinachotokea hivi sasa katika medani ya siasa ni sawa na hicho ambacho mwalimu amejaribu kukieleza katika kitabu chake hicho.
Kutokana na ugumu wa maisha unawakabili walio wengi ni wazi mgawanyiko sawa ambao ungetoa ahueni hiyo kwa wote na sio kundi fulani katika jamii.
Kupanda kwa bei za vyakula, mafuta ya taa, petroli na dizeli, ada za shule na gharama zingine ni wazi kuwa wawakilishi hao wa wananchi wanataka kuondolewa mashaka waliyonayo.

Mashaka hayo ni yale ambayo yanawafanya wafikiri kuwa uhuru ni wa kwao na sio wa watu wote kama lilivyokuwa lengo la kuutafuta kutoka kwa wakoloni.
Mwaka 2015 si mbali na huenda ukawa wakati mwafaka kwa wananchi kupitia masanduku ya kura tuwatoe mashaka na kuwaonyesha kuwa uhuru wetu ni wa wote na sio wa watu fulani.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Wednesday, 18 January 2012 10:14
 

Comments 

 
0 #1 2012-01-18 19:39
sioni sababu ya kuongeza hizo posho kwa wabunge'wakati madaktari wanakosa mishahara yao kwa muda unaotakiwa,wali mu pia ambao hawa ni watu muhimu ktk taifa letu embu tuongeze hizo posho kwa watu hawa kwanza then wengine baadae alafu tuone what next
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner