MwanzoContactsEmail
Home Makala Siasa Ukweli ni kwamba nchi za Afrika hazitajikwamua
BOOKMARK THIS PAGE
Ukweli ni kwamba nchi za Afrika hazitajikwamua  Send to a friend
Wednesday, 01 February 2012 13:01

Na Charles Kayoka MWALIMU Julius Nyerere alichukia sana na kutoa hotuba kali dhidi ya wale waliosema afadhali ya mkoloni kuliko serikali hii ya uhuru.

Sina uhakika angesema nini leo, miaka zaidi ya hamsini baada ya uhuru nchi za Afrika bado haziwezi hata kutengeneza sindano ya kufumia kitambaa, achilia kuwa ni chaka la kila aina ya ufisadi na dalili za
 kutojikwamua. Mimi sisemi afadhali ya mkoloni, bali nasema Afrika
 haitajikwamua!
 
Kwanza kuna tatizo la uongozi ambao kwa sasa umefunga ndoa na
 makampuni na serikali za nje. Wamekuwa wawekezaji ndani ya nchi zao
 kwa kujificha nyuma ya migongo ya wawekezaje, wana hisa huma, wamepata asilimia kumi, na wanashirikiana na wawekezaji kuwaibia wananchi wenzao. Kwa sababu hiyo sio rahisi wa kutumika kama nyenzo za kudhibiti wizi wa rasilimali za nchi.


Kama tulivyoona Zaire na kwingineko, nchi za wakubwa zikawatumia viongozi wa nchi zetu kuwafanya watu kuwa masikini zaidi.


 Linalokaribiana na uongozi ni kukosa kusema ukweli katika siasa na kwa
 sababu ya sekta ya siasa na serikali kuwa ndiyo sekta pekee yenye
 kipato cha uhakika na kukufanya uwe tajiri kwa haraka, wanaojiajiri
 huko ni wenyewe, na kwa lengo moja tu kutumia uongozi kwa malengo
 binafsi.


Matokeo yake ni kuona walio madarakani ni ndugu wa damu, wa
 ushemeji, wa familia, au wa urafiki tu. Na hapo hatuwezi kusemana wala
 kuambiana kuwa tumekosea. Hatutaendelea!
 Lakini unawezaje kujenga nchi ambayo haina mikakati kabisa ya
 kujikwamua ila ina mikakati tu ya kujikimu! Taifa linachofanya ni
 kusema bora twenda, na kesho ifike, lakini sio tutakuwa wapi miaka
 hamsini ijayo.


Namna gani tutakuza uchumi kwa kuweka mikakati minene
 ya uchumi. Naingalia Tanzania ambayo imezungukwa na nchi sita ambazo
 hazina bahari kabisa, na moja wapo haina miundo mbinu ya kibiashara na
 serikali yake kuu, lakini hatutumii hiyo kama fursa ya kujenga miundo
 mbinu ya kuvutia biashara na kuingiza fedha kwa wananchi na hivyo kodi
 zaidi kwa serikali.


Tatizo ni kuwa wafikiria maendeleo wetu huwa wanaishi jana na leo, na kutaka kuweka kidogo kwa ajili ya kuamkia kesho, hakuna wa kufikiria namna ya kufika mwakani. Hiyo ni kudra ya Mungu, hatupaswi kufikiria.
 Nchi za magharibi kina siku zinafikiria namna ya kupata maraisi na
 viongozi vibaraka hapa Afrika, na huwatumia hao kupata maslahi yao na
 kuyatetea.


Sasa imekuwa ni jambo la sifa kwa viongozi kujipendekeza
 kwa nchi za magharibi ili kupata kidogi kile kidondakacho kutoka meza
 ya bwana, lakini huyu bwana humega pande kubwa la rasilimali zatu na
 kuzihamishia kwake. Afrika inapata nini katika uhusiano huo usio na
 usawa, zawadi kidogo za magari, fedha za UKIMWI, kujengewa shule,
 kupea dawa za misaada, na nafasi za masomo ambazo mwanafunzi mmoja hatumii zaidi ya milioni kumi na tano kwa mwaka, na ikiwezekana


 wanamchukua pia akafanyekazi kwao. Afrika itawezaje kujikwamua.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner