
| Prof Omari: Tuige mfumo wa kikoloni kunusuru sekta ya elimu | Send to a friend |
| Tuesday, 24 January 2012 12:20 |
|
Hata hivyo, mhadhiri mwandamizi mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Issa Omari, pamoja na kusifu mafanikio hayo anasema mfumo wa sasa wa elimu haulingani kiubora na ule wa kikoloni. Akizungumza na mwandishi wetu Gedius Rwiza, Profesa Omari ambaye pia ni msomi bobezi wa fani ya elimu, anaeleza tofauti iliyopo kati ya elimu ya sasa na ile ya kikoloni. Kauli kuhusu mafanikio ya ujenzi wa shule, imekuwa ikitolewa sana na viongozi, lakini maendeleo ya kitaaluma yanazidi kuporomoka siku hadi siku. Swali: Kwa mtazamo wako, kitu gani kinachangia kuzorota kwa sekta ya elimu nchini? Kwa sasa mawaziri wanaochaguliwa siyo wataalamu wa elimu, badala yake wanapoingia madarakani kuiongoza sekta ya elimu, wanahesabu miaka iishe waondoke na siyo kuisimamia sekta ya elimu. Viongozi wote wanaoteuliwa hakuna mwenye utashi wa kuwakemea watu wanaokwenda kinyume na mahitaji muhimu katika sekta ya elimu. Ukifanya utafiti utakuta idadi kubwa ya viongozi waliopo katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, siyo wataalamu wa elimu jambo linalochangia kutopatikana kwa elimu bora. Kutokana na hali ya elimu kuendelea kuwa mbaya siku hadi siku, kuna kila sababu viongozi wote wanaoteuliwa kushika madaraka katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kuanzia Waziri,Makatibu Wakuu,Wakurugenzi pamoja na wafanyakazi wa ngazi za chini,wawe wamesomea taaluma ya elimu. Swali: Kuna tofauti gani kati ya elimu ya kikoloni na elimu ya sasa? Enzi zetu mwalimu wa somo alitakiwa alielewe vizuri,awe amelifaulu vizuri na utaratibu huo ulianzia darasani ambako wakuu wa shule na walimu wa taaluma walikuwa wanawaandaa wanafunzi ambao wangeweza kuwa walimu. Aidha, kila mwanafunzi aliyesikia anakwenda kuwa mwalimu, alijivunia hatua hiyo lakini sasa hivi mwanafunzi anayechaguliwa kwenda kuwa mwalimu, anajua anakwenda kuteseka. Hapo ndipo unapoweza kuona tofauti ya elimu ya kikoloni na sasa, maana mtu anayekwenda kuwa mwalimu akiwa kafeli na bado chuoni anapata alama za chini, unategemea mwanafunzi apate nini akifundishwa na mwalimu huyo? Asilimia kubwa ya walimu waliopo sasa hawawezi kupanua akili ya watu kuweza kusonga mbele na kuwa na ubunifu. Mtu mwenye uwezo mdogo, ni vigumu kumfanya mwanafunzi awe na uwezo mkubwa wa kufikiri, huku ni kuzidi kupotosha thamani ya mwalimu Lakini pia zamani sikuona mwanafunzi akikaa chini bila madawati, vifaa vya kufundishia na kujifunzia.Maabara zilitosha na sikuona mwanafunzi aliyemaliza kidato cha sita akiwa mwalimu bila kupata mafunzo rasmi ya ualimu. Hivi sasa mwanafunzi aliyemaliza kidato cha sita, utamkuta anafundisha sekondari hasa hizi za kata, jambo ambalo ni upotoshaji. Swali: Kwa mujibu wa maelezo yako,ualimu siyo fani ya kujivunia au? Alijivunia kuwa mwalimu na sio kwamba alikuwa mwalimu kutokana na kupata alama za chini, bali alikuwa mwenye uwezo mzuri na aliyefaulu vizuri, lakini kwa sasa hata thamani ya Mwalimu Nyerere imepotea. Jibu: Inawezekana endapo viongozi watakuwa na utashi na kukubali kubadilisha mtazamo kwamba kazi ya ualimu ni ya watu waliopata daraja la mwisho. Tunataka wanafunzi wanaokwenda ualimu wawe ni wale waliopata daraja la kwanza kama ilivyokuwa enzi zile ambapo mtu kuwa mwalimu alitakiwa kuwa amefaulu daraja la kwanza. Wasifu wa Profesa Omari Mwaka 1963 alijiunga na kidato cha sita katika Shule ya Sekondari Minaki, kabla ya kudahiliwa na Chuo Kikuu cha Dar es salaam alikosomea fani ya ualimu na baadaye kuajiriwa kama mhadhiri. |



MAADHIMISHO ya miaka 50 ya uhuru yamedhihirisha mafanikio ya kujivunia katika sekta mbalimbali ikiwamo elimu.Kwa mfano, katika sekta ya elimu ilielezwa kuwa nchi imepiga hatua kubwa katika ujenzi wa shule, vyuo na uandikishaji mkubwa wa wanafunzi katika madaraja mbalimbali ya elimu, jambo ambalo ni kinyume na ilivyokuwa enzi za ukoloni.











Comments
Totafakari!