
| 48 kwa 48 | Send to a friend |
| Monday, 16 January 2012 09:30 |
LONDON, EnglandMANCHESTER United imeifikia Man City baada ya kuizabua Bolton mabao 3-0 mwishoni mwa wiki katika mechi kali ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wake wa Old Trafford. Lakini Man City haikuwa na mchezo juzi wala jana, yenyewe inashuka dimbani leo Jumatatu kucheza na Wigan. Manchester imefikisha pointi 48 sawa na Man City iliyo kileleni ikiwa inajivunia tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa. Matokeo mengine, Tottenham inayoshika nafasi ya tatu, ilibanwa mbavu na kutoka sare ya 1-1 na Wolves katika mchezo uliokuwa wa ushindani. Tottenham sasa imefikisha pointi 46. Chelsea nayo imefikisha pointi 40 baada ya kuilaza Sunderland bao 1-0 kwa bao la Frank Lampard katika dakika ya 13. Arsenal inayoshika nafasi ya tano ilikuwa ugenini jana saa 1:00 usiku kukwaana na Swansea katika mchezo ambao Arsenal ilikuwa na mchezaji mwalikwa, Thierry Henry. Matokeo mengine ya mwishoni mwa wiki; Aston Villa ilitoka sare ya 1-1 Everton wakati Blackburn iliifumua Fulham 3-1. Liverpool na Stoke zilitoka suluhu na West Brom ilitandikwa mabao 2-1 na Norwich. |
| Last Updated on Monday, 16 January 2012 10:35 |



LONDON, England










