
| Man United vs Man City | Send to a friend |
| Monday, 30 January 2012 11:32 |
|
NI kama vile mechi ya Manchester United na Manchester City kunyang'anyana kiti. Mmoja akiteleza mwingine anachukua nafasi. Kwa sasa, Man City iko kileleni ikiwa na pointi 54 wakati Man United ina pointi 51. Ligi hiyo ambayo haikuwa na mechi mwishoni mwa wiki, itakuwa na mechi za upinzani kesho kwani kila mmoja anacheza muda mmoja, saa 5:00 usiku. Lakini tofauti iko kwa Man Utd ambayo itacheza na Stoke Uwanja wa Old Trafford wakati Man City watakuwa ugenini kuwafuata Everton. Hata hivyo, Stoke iliyo nafasi ya nane ikiwa na pointi 30 na Everton nafasi ya 14 na pointi 26, si timu za kubeza hata kidogo kwani zinaweza kufanya lolote lile katika mechi hizo. Swansea iliyoshtua kwa kuiadhiri Arsenal, itakuwa nyumbani kuwaalika Chelsea inayoshika nafasi ya nne kwa kuwa na pointi 41, nafasi ambayo haina kipingamizi kushushwa kwani hata Arsenal na Newcastle zikishinda hazitaiathiri. Arsenal itakuwa ugenini dhidi ya Bolton sawa na Newcastle iliyoalikwa na Blackburn huku kila mmoja akiwa na pointi 36. Mechi hizo zitachezwa keshokutwa. Tottenham inayokuja kwa kasi ikiwa na pointi 46, inataka kuisogelea Man United lakini endapo tu itaifunga Wigan inayoshika mkia wa ligi. Mechi nyingine ngumu kesho ni kati ya Wolves itakayokuwa mwenyeji wa Liverpool mechi itakayoanza saa 4:45 usiku. Mechi nyingine za Jumatano ni kati ya Aston Villa na QPR (4:45 usiku) wakati Fulham itapambana na West Brom huku Sunderland ikichuana na Norwich. Mechi zote zitachezwa saa 5:00 usiku. |














