
| Andrey Arshavin;Sasa ni adui no.1 Arsenal | Send to a friend |
| Monday, 30 January 2012 11:34 |
|
MWISHONI mwa wiki iliyopita, baada ya mechi ya Arsenal na Manchester United, jina la Andrey Arshavin lilichomoza na zaidi kuitwa adui namba moja wa Arsenal. Kadhia ilimkuta mchezaji huyo kwanza katika vyumba vya kubadilishia baada ya mchezo wa Manchester United, na Arshavin alikuwa amechanganyikiwa zaidi. Arshavin kwa kuwa hakuwa katika kiwango chake, alikuwa akilaumiwa na mashabiki na alipoingia tu, mashabiki wa United walishangilia huku kocha Aesene wenger akimtoa Alex Oxlade-Chamberlain aliyekuwa akiissaidia kwa kiasi kikubwa Arsenal. Ilikuwa siku mbaya kwa Arshavin, ambaye alikuja Arsenal akitokea Zenit St Petersburg kwa dau la pauni 12milioni. Arshavin alikuwa akionekana kama mmoja wa wachezaji nyota Ulaya, lakini kwa sasa anaanza kupoteza mwelekeo wake. Arsenal wako katika mpango wa 'kumpiga' chini kabla ya msimu wa usajili wa dirisha dogo kumalizika usiku wa kesho na Zenit wanaonekana kutaka kumsajili tena. Kulikuwa na kauli zilizojaa hasira baada ya mchezo wa United, na alikaa muda mrefu katika vyumba hivyo huku akitafakari kilichotokea uwanjani. Nahodha Robin van Persie na Wojciech Szczesny walikuwa wakimlaumu sana na walikuwa wakipiga kelele kwa kuwa kila mmoja alicheza kwa nguvu, kujituma na kila aina ya jitihada lakini si kwa Arshavin. Kocha wake, Wenger alikataa kumsema moja kwa moja Arshavin baada ya kumuingia na yeye pia analaumiwa kwa kuganya maamuzi ya kumtoa mchezaji bila mpangilio. United ilipata bao dakika saba baada ya Arshavin kuingia, na mchezaji huyo wa Russia alishindwa kumzuia Antonio Valencia aliyetoa majalo kwa Danny Welbeck. matokeo hayo yameifanya Arsenal kuwa katika hali mbaya ya kumaliza ligi katika nafasi ya nne bora. Ni kiwango cha soka cha Arshavin, kushindwa kujituma na kujitambua uwanjani ndiko kulikomfanya kila mmoja sasa kumchukua hatua itakayomfanya aondoke tu kwenye timu hiyo. Hata mazoezini wachezaji wenzake wamekuwa wakimkasirikia. Arshavin aliviambia vyombo vya habari vya Russia kwamba huenda akarudi nyumbani baada ya kushindwa kufanya vitu England. Wenger naye mara zote husimama kwa wachezaji wake na amekuwa akimtetea Arshavin hadharani, na hata alitetea uamuzi wake wa kufanya mabadiliko. Arsenal pamoja na hayo, bado haijasema wazi kama itamuuza Arshavin kwa sababu Gervinho kwa sasa hayyuko na timu kwa kuwa anaitumikia Ivory Coast katika Fainali za Afrika, lakini mkongwe wa Gunners, Ray Parlour alisema kuwa ni wakati wa kumtema kikosini. Parlour, alikuwa akizungumza na talkSPORT, akasema Arshavin: “Simtaki. "Arsene Wenger anafanya naye mazoezi, lakini ni lazima aangalie kipya kutoka kwake. “Arshavin anaonekana kama hataki kucheza. Sasa haieleweke labda ni kwa sababu hapati namba mara kwa mara. Sijui hali itakuwaje, lakini kwa jinsi mambo yanavyokwenda, inaweza kuwa heri kwa Arsenal na yeye mwenyewe. “Hapangwi mara kwa mara. Inawezekana ikamchanganya na inapotokea kapata nafasi, inakuwa hajiamini. “Aliingia lakini hakuwa mchezoni. Kama ningekuwa kocha, nisingemuingiza katika mechi ta United.” Kw aupande mwingine, Parlour alimpongeza Oxlade-Chamberlain. Alicheza vizuri, soka ya kuvutia, aliongeza. Nilionana Thierry Henry baada ya mchezo na kuniambia, 'Ni mambo mengine yule dogo.' He’s a massive prospect for Arsenal and England. Oxlade-Chamberlain anasema kuwa hakuwa na kipingamizi cha kutoka kw akuwa anaheshimu uamuzi wa kocha Wenger. Ilikuwa kitu kigumu kufanya vinginevyo nje ya kocha, anasema dogo huyo. “Ni vizuri kila mara ukatambua kuwa mashabiki wanafurahia kiwango chako ama vinginevyo, lakini mwisho wa yote uamuzi unakuwa wa kocha. yeye Arsene Wenger, ndiye kocha mkuu wa Arsenal. Amefanya mengi kwa klabu, amefanya mengi kwa wachezaji sasa atakachokiamua, sitakuwa na kipingamizi, nitaheshimu uamuzi wake. Oxlade-Chamberlain alikuwa akitarajiwa kuanza katika kikosi cha kwanza Arsenal katika mechi ya jana dhidi ya Aston Villa. |
| Last Updated on Monday, 30 January 2012 14:00 |














