
| Balotelli: Why always me? | Send to a friend |
| Monday, 30 January 2012 11:36 |
|
INAWEZEKANA alikuwa akituma ujumbe kwa namna yake. Katika mechi ya Manchester United ambayo City ilishinda mabao 6-1, Mario Balotelli alivaa fulani ya ndani iliyoandikwa Why always me? (Kwanini kila mara mimi?) na aliionyesha baada ya kufunga. Leo hii Balotelli amesimamishwa na Chama cha Soka England, FA mechi nne za Ligi Kuu kutokana na kucheza mchezo wa ovyo. Balotelli amesimamishwa kwa kumtimba kichwani mchezaji wa Tottenham, Scott Parker. Lakini yeye mwenyewe pamoja na wakala wake wamehoji hali hiyo, huku Balotelli akisema, Kwanini kila mara mimi? Balotelli, pamoja na wakala wake wanaamini kuwa hakumkanyaga Parker kwa makusudi. Kutokana na hali hiyo, wakala huyo anasema kuwa anaona kama vipi yeye na mchezaji wake waondoke, Manchester City kwa kuwa hawatendewi haki, ikiwemo kufungiwa mechi nne kwa kile kilichoelezwa kuwa alimtimba kichwani, Parker. Wakala wake huyo, Mino Raiola, anasema kuwa atazungumza na mchezaji wake kuona uwezekana wa kumhamisha katika klabu hiyo. Mario hawezi kufungiwa mechi nne, anasema Raiola. Haikuwa sawasawa na hiyo ni kutokana na shinikizo la Modric. Haikuwa faulo ya kudhamiria, Mario hakutaka kumuuza yeyote, hakumuona Parker, na huo ndiyo ukweli. Nataka kuliweka sawa hili, lakini wachezaji wa England wakicheza mchezo wa ovyo, hakuna kinachofanyikalakini angalia kwa wachezaji wa kigeni kama Balotelli au Kompany, walitiliwa ngumu. Ukiangalia, kuna kitu tofauti amefanyiwa Balotelli, kazi yangu ni kumlinda na kumtafutia pengine. Nitazungumza na City juu ya hili, sijaulizia bei ya Balotelli na kuna timu kama sita au saba zinamtaka. Nilizungumza na Mario mwenyewe kaniambia anataka kubakia England, lakini anashangazwa na mambo anayofanyiwa. Raiola pia alisema, mwamuzi, Howard Webb alikuwa anajitete kwa kile alichodai kuwa hakuona kilichotokea. Mwamauzi aliona kila kitu, kwa sababu alizungumza na Mario baada ya tukio lile, Raiola anasema. Balotelli alikosa mechi ya Carling Cup nusu fainali dhidi ya Liverpool, ambayo City ililala kwa mabao 3-2, na pia atakosa mechi ya Everton, Fulham na Aston Villa. |
| Last Updated on Monday, 30 January 2012 13:51 |














