MwanzoContactsEmail
Home Makala Spoti Mikiki SENEGAL; 'Simba wa Teranga' aliyekatwa mkia asubuhi
BOOKMARK THIS PAGE
SENEGAL; 'Simba wa Teranga' aliyekatwa mkia asubuhi  Send to a friend
Monday, 30 January 2012 13:44

FAINALI za Afrika zinaendelea kwenye mataifa ya Equatoria Guinea na Gabon, huku baadhi ya timu zikiwa zimemaliza hatua ya awali na chache kukamilisha ngwe yake kati ya leo na kesho.

Kikubwa ni kutolewa mapema kwa Senegal Simba wa Teranga katika fainali za mwaka huu, ikiwa ni moja kati ya mataifa yaliyokuwa yakipewa nafasi kubwa kutwaa ubingwa.

Kocha wa Senegal, Amara Traore anasema kuwa mpango wao ni kushinda mechi yao iliyokuwa ikipigwa jana dhidi ya Libya.
 
Timu hiyo haikutarajiwa kama inyekuwa nyanya licha ya kumaliza ya kwanza kwenye kundi lake, ilifungwa 1-2 na wenyeji Equatorial Guinea kaika mechi yao ya pili iliyochezwa  Estadio de Bata. Katika mchezo wa kwanza, ilipigwa mabao 2-1 na Zambia kwenye Uwanja huo.
 
Simba wa Teranga waliokuwa Kundi A hawana nafasi tena na ni timu ya kwanza kuaga ambavyo haikutarajia.
 
Tulijiandaa kwa mchezo. Kimsingi, ni kwamba hatukuwa na bahati. Tulipania kufanya vizuri katika fainali za mwaka huu. Ni maumivu kwa wachezaji wanaocheza kwa mara ya kwanza, anasema Traore.
 
Nahodha Mamadou Niang anasema kuwa bahati haikuwaangukia na ndiyo sababu ya kufanya ovyo katika mchezo huo.
 
Tulipata nafasi nyingi tulishindwa kuzitumia. Ni huzuni sana. Tuna vijana wazuri, na asilimia 70 wanacheza kwa mara ya kwanza, alisema nahodha huyo ambaye timu yake ilikuwa ikipewa nafasi ya ubingwa na Kocha wa Zambia, Herve Renard.

Senegal ilikuwa ikipewa nafasi kwa kuwa ilikuwa na nyota wakali kama Armand Traore, Mohamed Diame, Demba Ba ambaye ni mmoja wachezaji wanaotisha katika klabu ya Newcastle ya England.

Kiu ya ubingwa
Timu hiyo inayonolewa na mzalendo, Amara Traoré na kushika nafasi ya 44 katika ubora wa soka, ilianza fainali kwa kujiamini huku kocha wake akitoa tambo mbalimbali kutwaa ubingwa wa Afrika ambao haujawahi kutua nchini humo.

Tunakwenda kwenye fainali za Afrika na matumaini...tutatwaa ubingwa wa Afrika mwaka huu na kuweka histori,  alisema kocha wa timu hiyo iliyokuwa ikipewa nafasi pia na
Kocha wa Ghana, Goran Stevanovic, bosi wa zamani wa Olympique Marseille, Pape Diouf
na kocha wa zamani wa Nigeria, Stephen Keshi.

Itakumbukwa Senegal ilikera mashabiki wake kwa kushindwa kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika Ujerumani 2006, walionyesha soka ya kuvutia katika Fainali ya Afrika 2002, na walipoteza kwa penalti baada ya suluhu na Cameroon.

Mbali na kunolewa na kocha mzalendo, iliwatumia wachezaji wa zamani kama Ferdinand Colly, Henri Camara katika benchi la ufundi huku kikosi kamili kikiundwa na Makipa: Khadim N'Diaye (ASC Linguère), Pape Latyr N'Diaye (US Ouakam) na Bouna Coundoul wa New York Red Bulls.

Mabeki ni Omar Daf (Brest), Armand Traoré (Queens Park Rangers),  
Pape Diakhaté (Granada),  Souleymane Diawara (Marseille), Moustapha Bayal Sall (Saint-Étienne), Jacques Faty (Sivasspor), Kader Mangane (Rennes), Cheikh M'Bengue (Toulouse) na Ludovic Sané wa Bordeaux.

Viungo: Rémi Gomis (Valenciennes), Deme N'Diaye (Arles-Avignon), Mohamed Diamé (Wigan Athletic) na Guirane N'Daw wa Birmingham City.

Washambuliaji: Mamadou Niang (Sadd SC), Souleymane Camara (Montpellier),  
Dame N'Doye (Copenhagen), Papiss Cissé (Freiburg), Demba Ba (Newcastle United) na Moussa Sow wa Lille.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner