
| Miaka 50 ya makosa ya kisiasa yaliyopaswa kuepukwa | Send to a friend |
| Friday, 09 December 2011 13:23 |
|
Lawrence Kilimwiko Vyama vya ushirika vilivyokuwa wamejengeka na kuwahudumia wakulima kwa mafanikio makubwa vilisambaratishwa ili kutoa nafasi kwa bodi za mazao na mashirika mengine. Baada ya bodi hizi kushindwa, ushirika ukarejeshwa ijapokuwa mambo yalikuwa tayari yameharibika. Mtindo wa kufanya mabadiliko kwa majaribio umeligharimu sana taifa katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru iliyopita. Cha kushangaza ni kwamba mwisho wa siku watanzania wamejikuta pale pale alipowaacha mkoloni mwaka 1961. Wakati Tanganyika iliyojinyakulia uhuru wa bendera mwaka 1961, ilikabidhiwa Katiba ya Uhuru ambayo licha ya kuwa na dosari nyingi, ilikuwa imeainisha vizuri sana nafasi ya Bunge kama chombo cha uwakilishi wa watu na nafasi ya vyama vya siasa kama taasisi za kidemokrasia, ilikuwa bayana. Kasoro kubwa katika Katiba ya Uhuru ilikuwa ni kule kuendelea kumtambua Malkia kama mkuu wa nchi huru. Kwa maneno mengine, Tanganyika ilikuwa huru lakini siyo jamhuri. Hali kadhalika, kulikuwa na mkuu wa Serikali lakini siyo mkuu wa nchi. Katiba ya Uhuru pia haikuwa na vipengele vya haki za binadamu. Chini ya Katiba ya Uhuru , Bunge ndicho kilikuwa chombo chenye madaraka ya mwisho kuhusu mstakabali wa nchi. Serikali iliongozwa na Waziri Mkuu kutoka chama chenye wabunge wengi kupitia majimbo ya uchaguzi. Lakini kwa kutumia kisingizio cha kasoro ya Malkia kuendelea kuwa mkuu wa nchi iliyohuru, uongozi wa TANU badala ya kukifuta kipengele hicho tu, uliamua mwaka 1962 kuandika Katiba mpya kabisa. Badala ya Rais kuwajibika Bungeni kama ilivyokuwa imedhamiriwa awali sasa akapewa mamlaka ya kulivunja Bunge. Hoja iliyojengwa kuhalalisha mabadiliko hayo makubwa ya kikatiba, ilikuwa ni kwamba TANU ilikuwa inawakilisha wananchi wote kwa kuzingitia ushindi wa kishindo iliyoupata katika chaguzi mbili zilizotangulia. Faida ya mfumo wa vyama vingi ni kwamba watu wanakuwa na uhuru kubadilisha uongozi kwa kuvishindanisha vyama. Kile kinachoshindwa kinakaa pembeni na kujipanga upya. Hasara ya chama kimoja ni kujisahau na kufanya kazi kwa mazoea tu. Serikali ya TANU pia iliamua kuzifuta serikali za mitaa sambamba na kuufuta utawala wa machifu. Kwa kufuta serikali za mitaa Serikali ya TANU ilijikuta katika wakati mgumu sana wa kutoa huduma za msingi zilizokuwa zikitolewa na serikali hizo. Hata Mwalimu Nyerere alipata kukiri baada ya kustaafu kwamba lilikuwa ni kosa kubwa kuzivunja serikali za mitaa na kwamba kama angepewa nafasi ya kurudi madarakani, hilo ni eneo ambalo asingerudia kufanya kosa kamwe. Vyama vya wafanyakazi vilifutwa na badala ikaundwa jumuiya ya wafanyakazi liyowekwa chini ya mwavuli wa chama tawala. Hali kadhali, vyama vya ushirika navyo vilifutwa na badala yake ukaundwa muungano wa ushirika uliwekwa kama jumuiya ya chama tawala. Kwa upande wa wafanyakazi, wao waligeuka vibarua wa serikali wasiokuwa na sauti yo yote juu ya jasho lao. Ikumbukwe tu kwamba, mengi ya majengo makubwa na mazuri yaliyojengwa awali huko mikoani yalikuwa yamejengwa na vyama vya ushirika. Kwa upande, chama kikuu cha Nyanza kilichokuwa kinawahudumia wakulima wa pamba, kilikuwa kimeshamiri hadi kuwa ndicho chama kikubwa cha ushirika kuliko vyama vyote vya ushirika barani Afrika. Mpango huo ulihusu kuwahamisha kwa nguvu watu kutoka kwenye vijiji vyao vya asili na kuwapeleka kwenye vijiji vya ujamaa. Maelezo yaliyotolewa ilikuwa, ni kuiwezesha serikali kusambaza huduma za kijamii hasa elimu, maji na afya kwa wote. Watu walibomolewa nyumba zao na kuhamishiwa kwenyemaeneo yaliyokusudiwa hata kama hakukuwa na maandilizi. Watu waliliwa na wanyama poro na kuumwana na nyoka. Akina mama walijifungulia maporini huku mvua ikinyesha bila msaada. Watu walipoteza mifugo na mali nyingine walizokuwa wamezihangaikia kwa maisha yao yote. Mwisho wa zoezi ilielezwa kwamba watu takriban million 14 walikuwa wamehamishiwa kwenye vijiji vipatavyo 8,299 kote nchini. Athari nyingine iliuwa ni kushuka kwa uzalishaji wa mazao yote ya chakula na biashara. Viwanda vya korosho vilivyokuwa vimejengwa wakati huo vilishindwa kufanya kazi kwa kukosa korosho baada ya wakulima kuhamishwa mbali na mashamba yao. Lengo jingine la kujenga ujamaa pia lilifeli vibaya sana. Hata vile vijiji vilivyoweza kupata mafanikio vilisambaratika kutokana na ubadhirifu uliofanywa na mamlaka za mazao pamoja na ulafi wa viongozi wa kisiasa waliojenga tabia ya kula mali za vijiji bure. Makosa mengine ya kisiasa yaliyopaswa kuepukwa na serikali ya chama makini ni pamoja na uuzaji wa nyumba za serikali, ubinafsishaji wa mashirika ya umma pamoja na kuondoa miiko ya uongozi iliyokuwa imeainishwa wakati wa Azmio la Arusha. |



kwamba kwa kuyarekebisha imejikuta inarudi kule kule ilikotoka.










