MwanzoContactsEmail
Home Michezo Kandanda Kocha Sounders: Ngassa jifunze kukakaba
BOOKMARK THIS PAGE
Kocha Sounders: Ngassa jifunze kukakaba  Send to a friend
Friday, 29 July 2011 20:11

Sosthenes Nyoni
PAMOJA na kufanya vizuri kwenye majaribio na kufuzu kocha, Sigi Schmid wa Seattle Sounders amemtaka mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Azam, Mrisho Ngassa kujifunza kusaidia ukabaji.

Ngasa amepewa na timu hiyo ya Sounders nafasi ya pili ya kurudi tena Marekani na kujiunga nayo hapo mwezi  Februari mwakani wakati wa kipindi cha usajili wa dirisha dogo Amerika Kaskazini.“Unapokwenda sehemu kama Tanzania na unapomuona mtu mmoja aliyesimama juu ya mabega ya wenzake wote, utajaribu kujiuliza kwanini imekuwa hivyo,” alisema Schmid.

Jibu la haraka ni Ngassa pekee.

Mchezaji huyo mwenye urefu wa futi 5, anawezza kutumia kasi yake na ujanja wa kupenya mabeki na kutengeneza nafasi.  Hata dhidi ya Manchester United aliweza kutumia nafasi ndogo aliyopata kupiga shuti lililopaa kwa kuiba mpira mbele ya beki  Rio Ferdinand.

“Ngasa si mchezaji mkubwa, lakini nina uzoefu ya wachezaji wafupi kufanya vizuri hapa Seattle, hivyo sio jambo litalotusumbua.  Ni mchezaji mwenye kasi.  Nafikiri kasi yake akiwa kwenye eneo fupi ni kitu cha kipekee,” alisema Schmid. “Kiufundi, ni mzuri.  Anaweza kukokota mpira na kupiga mashuti vizuri.  Anaweza kusoma mchezo vizuri.  Nafikiri anahitaji kujirekebisha kwenye ulinzi zaidi, lakini ni mchezaji mzuri kwenye kushambulia na mwepesi wa kuzoeana na wenzake uwanjani hilo ni jambo zuri,” alisisitiza Schmid.

Kauli hiyo ya kocha wa Sounders inaungana na ile ya mwenzake wa Taifa Stars, Jan Poulsen aliyewahi kusema Ngasa anatakiwa kujifunza kukaba kama soka ya sasa inavyotaka ili aweze kuwa mchezaji aliyetimia.

Kusajiliwa kwa Ngassa na timu  hiyo inayoshiriki  ligi kuu ya Marekani kumekuja baada ya kufuzu majaribio aliyoyafanya katika kikosi hicho  kwa takribani mwezi mmoja.Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Azam, Nasoro Idrisa alisema taarifa zilizowasilishwa kwao na kocha wa Seattle,  Schmid, Ngasa alifanikiwa kufuzu majaribio yake ambapo ameruhusiwa kurejea nyumbani na kutakiwa kurudi nchini humo kwa ajili ya kusajiliwa  rasmi wakati wa usajili wa dirisha dogo ambao hufanyika Februari.

"Kimsingi tulikuwa tunawasiliana na kocha wa Seattle  muda wote wa majaribio ya Ngasa, lakini jambo zuri ni kwamba  alitupa taarifa ya Ngasa kufanikiwa katika majaribio na sasa anatakiwa kurejea nchini humo kwaajili ya kusajiliwa rasmi mwezi Februari wakati wa kipindi cha usajili wa dirisha dogo.

"Tunamtarajia atatua nchini leo na kuendelea na majukumu katika klabu yake kama kawaida na hivyo ndivyo tulivyokubaliana toka awali,"alisema Idrisa.Aliongeza kuwa kwa upande wao hakuna kikwazo ambacho kinaweza kumzuia  Ngasa kutimiza ndoto zake na klabu yake akisema anaamini pande zote zitaafikiana katika suala la kiwango cha fedha za mauzo ya nyota huyo.

"Jambo muhimu kwanza tunashukuru amefanikiwa na ndio kitu muhimu kwani suala la makubaliano katika bei ya kumuuza sidhani kama ni tatizo, naamini pande zote mbili zitaafikiana,"alisema Idrisa.

Baraza la vyama vya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) limewataka wachezaji wa ukanda huu kuiga na kufuata nyayo za mchezaji  Mrisho Ngassa  ambaye hivi karibuni aliweka historia kwa kuchezea timu ya Seattle Sounders ya Marekani dhidi ya Manchester United ya England.Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye alisema kuwa bidii aliyoonyesha Ngassa ni mfano wa kuigwa kwani ameweza kucheza mechi dhidi ya timu bora duniani huku akiwa hajasaini fomu yoyote ya usajili.

Musonye alisema kuwa hatua ya Ngassa kucheza mechi hiyo ni faraja kwa Tanzania na ukanda wa soka wa Afrika Mashariki na Kati kwani ndiyo kanda pekee katika bara la Afrika linaloshindwa kufanya vyema katika mashindano mbali mbali.

Alisema Ngasa ni miongoni mwa wachezaji nyota kama Macdonald Maliga na Denis Oliech ambao wanacheza Italia na Ufaransa wakati Ukanda huu una wachezaji wengi ambao wana uwezo wa kufanya vyema, lakini wanashindwa kutokana na kukosa ari ya kufanya hivyo.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Friday, 29 July 2011 22:09
 

Comments 

 
0 #12 2011-08-01 06:25
sasa wewe unaongea lugha gani?Quoting Hamidu:
Quoting JOSEPH MWIJAGE NTEGA:
niwapongeze viongozi wa african lion kwani mara walipopewa hiyo nafasi hawakujari mchezaji anatokea timu gani bali waliangalia kiwango cha mchezaji.

pole kumbe hata mpira wa tanzani huujui... african lyon ndio nini?? Acha kumshusha Ngassa
Quote
 
 
0 #11 2011-08-01 02:57
kaa chini tengeneza programmu ya kujiendeleza hayo maeneo ulipokua na mapungufu ili ukifika mwezi wa 2 mwakani unaenda zako marekani kutuwakilisha. Inawezekana!!
Quote
 
 
0 #10 2011-07-31 21:08
hongera ngasa kazi uzi kwani hakuna mazuri bila jasho dogo
Quote
 
 
0 #9 2011-07-31 16:44
Ngasa hiyo ndio nafasi ya kutoka katika umaskini juhudi zinahitajika
Quote
 
 
-1 #8 2011-07-31 10:01
HAKIKA UNGEBAKI WA BONGO KAMA KANAVARO KAMA USINGESHTUKIA YANGA
Quote
 
 
+1 #7 2011-07-30 20:44
Hizi habari hazijakomaa kam kweli ngassa kafuzu au ni kututuliza tuu watanzania wenye kiu ya kuona vijana wetu wanapata ajira nchi za nje. Hata Tomas Ulimwengu aliandikwa andikwa hivi hivi na mpaka leo haijulikani kaishia wapi.Uwezo wa ngassa ni wa hali ya juu sana na kasi yake ni ya kusisimu kama vile Ronaldo. Kinacho tuponza kwa wachezaji wetu ni jina letu katika medani ya soka katika FIFA. ni vigumu sana wachezaji wetu kupata ajira katika vilabu vya marekani na Ulaya kama nchi yetu ina shika nafasi za 97- 130. Hivyo TFF inatakiwa kuchagua kocha mwenye hadhi ya kufundisha mpira wa ngazi za ligi kuu brazil na Ulaya na sisi tutapa nafasi nzuri za kati ya 12-40. Mimi natoa lawama zote kwa TFF kutochagua kocha wa dalaja la kwanza. Matokea yake vijana wetu kama kina ngassa wanpangwa dakika kumi kabla ya mpira kuisha. Ngassa wewe endelea kutafuta timu tuu na ipo siku utafanikiwa. nakuombea sana.
Quote
 
 
-2 #6 2011-07-30 16:28
dogo Ngasa tatizo anapupa,na kukimbiakimbia, yele yale niyowahi kuyasema sasa yamtokea,soka bongo ni magutu maguto
Quote
 
 
-5 #5 2011-07-30 12:08
Quoting JOSEPH MWIJAGE NTEGA:
niwapongeze viongozi wa african lion kwani mara walipopewa hiyo nafasi hawakujari mchezaji anatokea timu gani bali waliangalia kiwango cha mchezaji.

pole kumbe hata mpira wa tanzani huujui... african lyon ndio nini?? Acha kumshusha Ngassa
Quote
 
 
+2 #4 2011-07-30 11:01
niwapongeze viongozi wa african lion kwani mara walipopewa hiyo nafasi hawakujari mchezaji anatokea timu gani bali waliangalia kiwango cha mchezaji.
Quote
 
 
0 #3 2011-07-30 10:19
Wewe ni mfupi kama Daud, nae mungu amekuona. Hakika mie ni miungoni mwa watz tunaokuombea kila lililo jema. Mungu afungue ufahamu wako ili uitangazie dunia kuwa tanzania ni nchi kama nchi zingine katika medani za soka.

Mungu mbariki ngassa, Mungu ibariki tanzania. AMINA
Quote
 
 
0 #2 2011-07-30 08:33
Ngassa,mshukuru Mungu kwa hiyo nafasi ya kucheza Marekani.Ungeng'ang'a nia YANGA soka la kulipwa ungelisikia kwenye TV na INTERNET tu,
Quote
 
 
0 #1 2011-07-30 07:19
kila lililo na kheri Ngasa ukomboe soka la bongo
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner