
| Poulsen kuwapa darasa makocha | Send to a friend |
| Saturday, 28 January 2012 09:23 |
|
Vicky Kimaro Boniface Wambura, Ofisa habari wa TFF, alisema kozi hiyo imepangwa kuanza Februari 12-25 na kwamba sifa za waombajji ni wale wenye elimu kuanzia ya kidato cha nne. "Jan Poulsen ni mkufunzi wa Shirikisho la Soka Ulimwenguni (Fifa), atasaidiana na Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Sunday Kayuni ambaye pia ni mkufunzi wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na Kocha wa timu za Taifa za vijana, Kim Poulsen ambaye pia ni mkufunzi wa Chama cha Mpira wa Soka Denmark (DBU)," alisema Wambura. Alisema lengo ni kuendeleza programu ya kuwanoa makocha nchini ili waweze kuinua vipaji vya vijana kwa maendeleo ya soka la Tanzania. Wambura alisema mwisho wa kupokea maombi kwa makocha wanaotaka kushiriki kozi hiyo ambayo ada yake ni sh60,000 itakuwa Februari 5 mwaka huu. "Sifa kwa waombaji ni elimu ya kuanzia kidato cha nne, wawe wanafanya kazi ya ukocha na kufaulu vizuri mafunzo ya ukocha ngazi ya kati (intermediate level). Pia wawe wamefundisha angalau kwa miaka miwili baada ya kupata cheti cha Intermediate level." alisema Alisema pia, maombi yawe yameidhinishwa na, ama vyama vya makocha wa mpira wa miguu vya mikoa, Vyama vya Soka wilaya au Vyama vya Soka Mikoa. Makocha watakaofaulu kozi hiyo watapata sifa ya kuhudhuria kozi ya ukocha leseni C ya CAF. |













