MwanzoContactsEmail
Home Michezo Kandanda Okwi atoa zawadi kwa Simba
BOOKMARK THIS PAGE
Okwi atoa zawadi kwa Simba  Send to a friend
Thursday, 02 February 2012 22:00

Imani Makongoro
MSHAMBULIAJI wa Simba, Emmanuel Okwi amesema mabao mawili aliyoifungia timu yake juzi dhidi ya JKT Oljoro ni zawadi kwa mashabiki wa klabu hiyo.

Okwi alifunga mabao hayo katika kipindi cha pili alipoingia kuchukua nafasi ya Gervais Kago, ambapo alisema alikuwa na nia ya kulipa fadhila kwa mashabiki wa mabingwa hao mara 16 wa Tanzania kutokana na kuthamini mchango wake.

"Mbali na mashabiki pia ni zawadi kwa kocha wangu, Cirkovic Milovan licha ya kuchelewa kujiunga na mazoezi bado alinipa nafasi katika mechi ya leo 'juzi' na kufanikiwa kufunga mabao mawili,"alisema Okwi.

Okwi alisema mbali na ushindi huo watahakikisha wanaendelea kucheza kwa kiwango cha juu hadi mwishoni mwa msimu huu na kupeleka kombe la Ligi Kuu Msimbazi.

"Mechi ilikuwa ngumu na kipindi cha pili wapinzani wetu walionekana kutulia na kujiamini, lakini ushirikiano na kuelewana kati yetu ndio siri ya ushindi wetu licha ya kuwa tulikuwa pungufu," alisema Okwi.

Mabao hayo mawili yanafanya Okwi kufikisha mabao saba akiwa nyuma kwa magoli matatu kwa mshambuliaji wa Azam, John Boko aliyefunga (10) wakati Kenneth Asamoah akishika nafasi ya pili kwa kuzifumania nyavu mara tisa, Gaudence Mwaikimba wa Azam (6) huku Hamis Kiiza (Yanga), Mohamed Kijuso (Villa Squad), Enyinna Darlington (Toto) na Juma Semsue (Polisi) wamefunga mabao matano kila moja.

Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 34, tatu zaidi ya wapinzani wao wa Jadi, Yanga (31) huku wakifutiwa kwa karibu na Azam yenye pointi 29 wakati klabu hizo tatu zikiwania kusaka ubingwa.

Vita kubwa ipo mkiani kwa Villa Squad yenye pointi 10, Polisi Dodoma (11), Toto African (13) na Coastal Union (14) zinazosaka kujiengua na baa la kushuka daraja msimu huu.

Ligi Kuu Tanzania Bara itaendelea tena Jumamosi na Jumapili, ambapo Jumamosi,  Villa Squad itacheza na Simba kwenye uwanja wa Taifa, Moro United itacheza na Coastal Union kwenye uwanja wa Chamazi na Ruvu Shooting itacheza na Polisi Dodoma huko Mlandizi.

Siku ya Jumapili kutakuwa na mechi kati ya Azam na Oljoro kwenye uwanja wa Chamazi, wakati Toto Afrikacan itaikaribisha African Lyon kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza huku Kagera Sugar ikiikaribisha JKT Ruvu kwenye uwanja wa Kaitaba.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #1 2012-02-04 11:34
hongera Okwi kwa kuwaonesha mfano wachezaji wa kitanzania ni jinsi gani mchezaji anatakiwa kujituma....
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner