
| Yanga yahofia usalama Misri | Send to a friend |
| Saturday, 04 February 2012 09:12 |
|
Kalunde Jamal Akiongea na Mwananchi jana, Katibu Mkuu wa Yanga, Selestine Mwesigwa alisema kuwa hali ya usalama wa viwanja nchini humo si shwari kutokana udhaifu katika ulinzi. "Usalama ni mdogo, tunaliomba Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kufuatilia kwa karibu hali ya usalama nchini humo kabla ya sisi kwenda kucheza," alisema Mwesigwa. Anasema amefurahishwa na hatua ya TFF ya kushtushwa na jambo hilo, lakini imewataka wasiishie kushitushwa tu bali wachukue hatua kwa kuonyesha vitendo. Mwesigwa alisema hata kabla ya maafa hayo, hali ya usalama kwenye viwanja vingi nchini Misri si shwari na kukumbushia mechi waliyocheza miaka ya nyuma dhidi ya Al Ahli ilibidi ulinzi kuongezwa. "Nashukuru mechi ya kwanza itakuwa nyumbani, hofu yetu ni mechi ya marudiano itakayochezwa ugenini. TFF ishirikiana na Shirikisho la soka Afrika (CAF) kuhakikisha kunakuwapo na ulinzi wa kutosha," alisema Mwesigwa. Juzi usiku zaidi ya mashabiki 74 waliuawa wakati wa vurugu za mashabiki kwenye Uwanja wa Port Said wakati wa mechi iliyozikutanisha timu za Al Ahly na Al-Masry. |















Comments