MwanzoContactsEmail
Home Michezo Kandanda Wambura, TFF waendelea kusutana
BOOKMARK THIS PAGE
Wambura, TFF waendelea kusutana  Send to a friend
Saturday, 04 February 2012 09:13

Jessca Nangawe
BOSI Mtendaji wa zamani wa kilichokuwa Chama cha Soka Tanzania (FAT), sasa Shirikisho la Soka (TFF), Michael Wambura ameibuka na kusema shirikisho hilo linajichanganya kwa kushindwa kuitambua vyema katiba yake.

Kauli ya Wambura imekuja siku moja tangu Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah kusema shirikisho lake linatafuta ufafanuzi wa kisheria wenye lengo la kuondoa mkanganyiko katika utendaji wa kazi wa kamati zake kama ilivyotokea hivi karibuni.

Wambura mbali na kuibeza TFF, ameseme atapinga kufanyika uchaguzi mkuu wa Chama cha soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) mpaka hapo marekebisho ya katiba yatakapofanyika. Uchaguzi huo umepangwa kufanyika Machi 18.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Wambura alisema Shirikisho hilo haliko makini na limeshindwa kuilewa katiba yake na matokeo ni kushindwa kutoa uamuzi sahihi.

Alisema kimsingi malalamiko yake hayakupaswa kupitiwa na Kamati ya Hadhi za Wachezaji kwa vile Kamati ya Rufaa ndiyo yenye uamuzi wa mwisho kutengua uamuzi ya kisheria.

"Utendaji kazi TFF una mashaka makubwa, inashangaza viongozi wake badala ya kwenda mbele wanarudi nyuma. Wanashindwa kujua kwamba kamati ya mwisho ni ile ya Rufaa," alihoji Wambura.
Aliongeza: "Nashangaa suala langu lijadiliwe na Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji huu ni upotoshaji na udanyanyifu.

Mimi wakati nakata rufaa nilikwenda ngazi kwa ngazi, nilianza Kamati ya Nidhamu mpaka ngazi za juu. Ni lazima sheria zifuatwe ili kuwapo na maelewano mazuri."
Alisema atawasilisha barua Jumatatu ijayo kupinga uchaguzi wa DRFA kutokana na kutofanyika kwa marekebisho ya katiba na kushindwa kufuata katiba iliyowekwa na TFF.

Katika barua ya TFF kwenda kwa vyama vya Mikoa iliyotolewa hivi karibuni na Osiah ilivitaka vyama vyote kuhakikisha vinarekebisha katiba zao ili ziendane na katiba ya mfano ya TFF kwa kutekeleza maagizo hayo na kutimiza wajibu wa kikatiba kwenye katiba ya TFF ibara ya (12) (d) (e) na (n).

"Vyama vyote vinatakiwa kulipa ada ya shilingi lakimbili lakini wenzetu wa DRFA wanalipa lakitano hii inadhihirisha kuna upotoshaji ndani ya unaopelekea kutokwenda sawa na katiba," alisema.

Akiongelea madai hayo ya Wambura, Osiah alikanusha na kusema wanachokifanya wao ni kuomba ushauri wa kisheria na hiyo haina maana kwamba hawaifahamu katiba yao.

Kuhusu kupinga Uchaguzi Mkuu wa DRFA, alisema wameshawasiliana na chama hicho kutaka wapewe mchakato mzima kuelekea uchaguzi mkuu ili kuangalia upya vipengele vinavyohusika na uchaguzi na kuvifanyia marekebisho.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #1 2012-02-04 12:14
Sioni tatizo la hawa TFF kumbania Wambura kushiriki kwenywe chaguzi mbalimbali hapa lazima kuna tatizo upande wa TFF cjui wanahofia nini....Osiah anaweza kupingana na kamati halali zilizowekwa kikatiba kama anaona suala lina utata alipeleka mkutano mkuu ndio utatoa maamuzi sahii na sio kwenda tena kuomba ushauri kwenye kamati nyingine na akumbuke yeye yupo kwenye sekretarieti na sio muamuzi wa mambo yote bali ni utendaji wa shirikisho
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner