MwanzoContactsEmail
Home Michezo Kandanda Kumekucha Ligi Daraja la kwanza
BOOKMARK THIS PAGE
Kumekucha Ligi Daraja la kwanza  Send to a friend
Saturday, 04 February 2012 09:15

Jessca Nangawe
MZUNGUKO wa pili wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inayochezwa katika makundi matatu tofauti unaanza leo kwa michezo sita kufanyika katika viwanja mbalimbali hapa nchini.

Akitangaza ratiba hiyo Afisa habari wa Shirikisho la soka Tanzania TFF, Boniface Wambura alisema katika Kundi A, Morani FC itakuwa mwenyeji wa Burkina Faso ya Morogoro katika mchezo utakaochezwa Kiteto mkoani Manyara huku kwa upande wa Kundi B timu zote sita zitakuwa uwanjani.

Kwa upande mwingine Wambura alisema timu ya Small Kids ya Rukwa itacheza na Polisi ya Iringa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Mbeya City na Tanzania Prisons zitaumana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya na Majimaji na Mlale JKT watapepetana katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Kundi C litaanza kwa mechi mbili ambapo AFC ya Arusha watakuwa wageni wa Manyoni mkoani Singida na Rhino na Polisi Tabora zitakwaruzana kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

Mechi nyingine ya kundi hilo itakuwa kati ya 94 KJ na Polisi Morogoro itachezwa kesho kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi Mkoani Pwani.

"Timu zote tayari zimejiandaa kuanza kwa ligi hiyo na tayari zimewasili katika mikoa yao na baadaye timu tisa zitasonga mbele kwenye ligi ndogo ya kupata timu tatu zitakazopanda Ligi Kuu msimu ujao," alisema Wambura.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner