
| Wachovu Villa Squad kuijaribu Simba | Send to a friend |
| Saturday, 04 February 2012 09:17 |
|
Sosthenes Nyoni Mbali ya kipute hicho kitakachowakutanisha 'watoto wa mjini', vumbi la ligi hiyo pia litakuwa linaendelea kwenye Uwanja wa Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, pale Moro United watakuwa wenyeji wa Coastal Union ya Tanga, wakati maafande wa Ruvu Shooting watakuwa wakipepetana na wenzao wa Polisi Dodoma kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi Pwani. Katika mzunguko huo wa 16 wa Ligi Kuu unaanza leo kwa timu sita kushuka dimbani na ushindi kwa Simba watawasafishia njia kwa kuweka tofauti ya pointi saba dhidi ya mabingwa watetezi Yanga ambao wenyewe watashuka dimbani Jumatano kuivaa Mtibwa Sugar. Mabingwa wa Kombe la Mapinduzi, Azam wenye ndoto ya kutwaa ubingwa msimu huu watashuka dimbani kesho kuivaa JKT Oljoro, huku Kagera Sugar watakuwa nyumbani Kaitaba kuivaa JKT Ruvu. Simba iliyojiimarisha kileleni na pointi zake 34 baada kuendeleza ubabe dhidi ya JKT Oljoro, itakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuibuka na ushindi wa pointi tatu dhidi ya Villa Squad.Safu ya ushambuliaji wa Simba imeimarika zaidi baaada ya kupona majeruhi kwa nyota wake wa kimataifa kutoka Zambia, Felix Sunzu pacha wa Emmanuel Okwi. Ushirikiano wa Sunzu na Okwi umetoa faida kubwa kwa Simba kwani wawili hao kwa pamoja wamefunga mabao 11 kati 25 yaliyofungwa na timu hiyo msimu huu.Kwa upande mwingine, licha ya kocha wa Simba, Milovan Cirkovic kufurahia kurejea kwa Sunzu pia atakuwa katika majonzi ya kumkosa kiungo wake'mtukutu' Haruna Moshi 'Boban' anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoonyeshwa wakati wa mechi dhidi ya JKT Oljoro. Hata hivyo pamoja na majonzi hayo ya kukosa huduma ya Bobon, bado Cirkovic atajivunia uwapo wa viungo wengine kama Mwinyi Kazimoto, Jonas Mkude na Uhuru Seleman ambapo hakuna shaka kwamba watakuwepo kikosini. Villa Squad inayoburuza mkia kwenye msimamo, iko nyuma kwa tofauti ya pointi 24 dhidi ya Simba lakini inaonekana kutokata tamaa na inaweza kufanya lolote mbele ya Simba. Licha ya Simba kupewa nafasi zaidi ya kuibuka mbabe, matokeo yasiyotarajiwa na wengi si ajabu ikiwa yatatokeo kwani ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Toto Africans ilioupata Villa Squad katika mechi yake ya mwisho yanaweza kuamsha morali ya wachezaji wa timu hiyo katika kusaka mafanikio zaidi. Pamoja na matatizo yao ya nje ya uwanja Villa watakuwa na silaha moja kubwa ni mshambuliaji wao Mohamed Kijuso aliyefunga mabao 5 msimu huu. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba atakuwa na kazi ya kuhakikisha anaifungia timu yake ya Villa bao ili kuingia kwenye orodha ya nyota wanaowania tuzo ya ufungaji bora. Wakati huohuo, Uongozi wa Simba kupitia kwa msemaji wa klabu hiyo Ezekiel Kamwaga umeliandikia Shirikisho la Soka Tanzania(TFF)ukipinga kitendo cha aliyekuwa mwamuzi wa mechi yao na JKT Oljoro kumwonyesha kadi nyekundu Boban. "Tumeiandikia barua TFF kupinga adhabu ya kadi nyekundu ya Boban, kimsingi tumetazama mechi ile kupitia mkanda wa video tumebaini hakucheza rafu yoyote," alisema Kamwaga. Katika hatua nyingine pambano la ligi kuu kati ya Simba na Oljoro JKT lililochezwa katikati ya wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 40,191,000. Afisa habari wa TFF, Boniface Wambura alisema jana kuwa baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kila timu ilipata sh. 7,023,171, uwanja sh. 2,341,057, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 936,423, TFF sh. 2,341,057, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,170,528 na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 234,106. |














