MwanzoContactsEmail
Home Michezo Kandanda Wachezaji Yanga kuonja machungu ya kodi
BOOKMARK THIS PAGE
Wachezaji Yanga kuonja machungu ya kodi  Send to a friend
Thursday, 02 September 2010 21:38

Vicky Kimaro
UONGOZI wa Yanga utakutana na wachezaji wao mapema wiki ijayo kwa lengo la kuwaelimisha utaratibu mpya wa makato ya kodi ya serikali kutoka kwenye mishahara yao.

Akizungumza na Mwananchi, Mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga alisema kamati yake itakutana wiki ijayo kuzungumzia masuala mbalimbali pamoja na kukaa na wachezaji hao kuwaelimisha kabla ya kuanza zoezi hilo.

"Tulishakutana na Mamlaka ya Kodi ya Mapato Tanzania, TRA, na kujadiliana nao wakatuelimisha, sasa ni jukumu letu na sisi kuwaelimisha wachezaji wetu ili nao waanze kuichangia serikali yao kwa kipato wanachokingiza,"alisema Nchunga ambaye kwa taaluma ni mwanasheria.

"Unajua kipato chochote halali ni lazima kikatwe kodi, sasa hatuwezi kuwashtukiza kwa kuwakata bila kuwaambia chochote italeta mtafaruku mkubwa, ukizingatia huko nyuma hawakuwahi kufanyiwa hivyo, tutawaelimisha taratibu na natumaini watatuelewa," alisema Nchunga ambaye alidai zoezi la kukatwa kodi litaanza muda si mrefu kuanzia sasa.

Akizungumzia kuhusu kuwakatia wachezaji wao mafao ya NSSF Nchunga alisema "Hii tupo kwenye mchakato lakini tunaanza kwanza na hili la TRA wakishatuelea ndio tutawaelimisha pia na NSSF ili wajue kuna vitu kama hivi ambayo wanastahili kuchangia na kuvipata."alisema

"NSSF ni haki yao ya msingi ambayo ni lazima wapate kama mfanyakazi mwingine yoyote yule, hii ni nzuri kwani wanakatwa kiasi fulani na klabu inawachangia kiasi fulani itawasaidia kwa maisha yao ya baadae."alisema.

Naye Calvin Kiwia anaripoti kuwa mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Iman Madega amewataka mashabiki na wadau wote wa soka nchini kuiombea dua timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ili ifanye vizuri mchezo wake na Algeria utakaofanyika leo kwenye mji wa Algiers saa 4:00 usiku sawa na saa 7:00 za usiku.

Stars itapambana na Algeria katika mchezo huo wa kwanza kuwania kufuzu fainali za Afrika 2012 zitakazoandaliwa kwa pamoja kati ya Guinea ya Ikweta na Gabon

Madega aliliambia Mwananchi jana kuwa Watanzania wote hawana budi kuiombea dua timu yao ili iweze kushinda mchezo huo na kujiweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele.

Stars imepangwa kundi D kwenye mashindano hayo ikiwa na timu za Morocco na Afrika ya Kati.

Wakati huo huo, uonjgozi wa Yanga kesho Jumamosi utakutana na makatibu na wenyekiti wa matawi yao yote ya Tanzania kwa ajili ya kujadili maendeleo ya klabu na ushiriki wa timu katika Ligi Kuu inayoendelea.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner