|
Matumla amfunga mdomo Cheka |
Send to a friend |
|
Monday, 02 January 2012 21:46 |
|
Juma Mtanda na Masoud Masasi,Morogoro BONDIA Mohamed Matumla amemjibu kwa vitendo Cosmas Cheka baada ya kumchapa kwa pointi 231 dhidi ya 225 juzi katika pambano lisilokuwa la ubingwa lililofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Ushindi huo wa Mohamed umechukukiwa kama kulipiza kisasi baada ya baba zake Rashid na Hassan Matumla mara kadhaa kupokea kipigo kutoka kwa bondia Francis Cheka wa Morogoro.
Mohamedi ambaye ni mtoto wa kwanza wa Rashidi Matumla alifanikiwa kufuta aibu hiyo baada ya kumchapa Cheka kwa pointi 231 dhidi ya 225.Katika pambano hilo la uzito wa chini wa kilo 57 liliamuliwa na majaji watatu ambapo jaji namba moja Anthony Ruta alitoa alama 77 kwa Matumla na 74 kwa Cheka, jaji namba mbili Agapeter Mnazareth akitoa 76 kwa Matumla wakati Cheka akipata alama 74 na jaji namba tatu Emmanuel Mlundwa akitoa 77 kwa Matumla na 74 kwa Cheka.
Cheka alianza vizuri katika raundi tano za mwanzo kwa mshushia makonde mazito mpinzani wakwe na kumdondoka chini mara moja katika raundi tano za kwanza.Matumla alijibu mapigo katika raundi tatu za mwisho kwa kumtandika vilivyo Cheka hadi kuanza kucheza rafu kwa kumpiga kichwa Matumla.
Akizungumzia pambano hilo Rais wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (PST) Emmanuel Mlundwa alisema kuwa katika pambano hilo mabondia wote walicheza vizuri, lakini kitendo cha Cheka ya kumpiga kichwa Matumla ilisababisha kupokonywa pointi zilizofanya kukosa ushindi. Katika mapambano ya utangulizi bondia Mkulu Katoto alitoka sare na Mohamedi Matimbwa, huku pambano la wanawake Asha Nzoa akimchapa kwa pointi Salma Kihobwa 38-40, huku Jamila Matimbwa alimchapa kwa KO Mariam Abdallah katika raundi ya pili.Pambano hilo lilihudhuriwa na mashabiki wengi akiwemo mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera.
|