MwanzoContactsEmail
Home Michezo Ngumi PST yamsimamisha kazi Mnazareth
BOOKMARK THIS PAGE
PST yamsimamisha kazi Mnazareth  Send to a friend
Monday, 16 January 2012 12:05

Imani Makongoro
SHIRIKISHO la ngumi za kulipwa Tanzania (PST), limemsimamisha makamu wake wa rais, Agapeter Mnazareth kufuatia kujihusika kwake na pambano la Karama Nyirawila dhidi ya Francis 'SMG' Cheka.

Kwa mujibu wa barua iliyosainiwa na rais wa PST, Emmanuel Mlundwa yenye namba VP/2012/1, bodi ya PST iliamua kumsimamisha Mnazareth kuendelea kuwa makamu wake wa rais hadi pale uchunguzi utakapokamilika.

PST iliamua kumsimamisha kufuatia kumtuhumu Mnazareth kuwa match maker wa pambano la Nyirawila na Cheka huku akielewa kufanya hivyo kumeigharimu nchi kupoteza mkanda WBF aliovuliwa Nyirawila.

“Tumemsimamisha na sasa yuko katika uchunguzi endapo tutagundua anahusika katika hilo hatutakuwa tayari kufanya naye kazi hivyo atakuwa amejiondoa moja kwa moja PST," alisema  Mlundwa.

Hata hivyo, Mnazareth alisema yeye aliamua kumsaidia Philemon Kyando ambaye ndiyo muandaaji wa pambano hilo kutafuta mabondia ambao watachuana hadi kuwapata Cheka na Nyirawila.

Alisema yeye ni 'match maker', na kufanya hivyo ni kazi yake na kusisitiza hata Mlundwa ni 'match maker' nje ya nchi hivyo yuko tayari kwa maamuzi yoyote.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner