
| Cheka amchapa Nyilawila | Send to a friend |
| Monday, 30 January 2012 14:31 |
Lilian Lucas,MorogoroBONDIA aliyejivua ubingwa wa dunia (WBF), Kalama Nyilawila juzi alishindwa kwa pointi na bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Francis Cheka katika pambano lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoano Morogoro. Katika pambano hilo lililokuwa la raundi 10 na lilihudhuriwa na mashabiki wengi, Cheka alimshinda Nyilawila kwa pointi 298 kwa 289. Muda wote bondia Cheka alionekana kutawala pambano, ambapo mpinzani wake Nyilawila alionekana kuzidiwa na makonde mazito ya Cheka, ambapo Nyilawila naye aliendelea kumtunishia misuli kwa kutaka kuonekana kuwa ubingwa wa dunia haukuwa wa kubahatisha. Katika raundi ya 1,2, 3 mabondia hao walionekana kuwa na kiwango sawa, ilipofika raundi ya 6, 7, 8, 9 na 10 Francis Cheka alionekana kumzidi nguvu Bondia Kalama Nyilawila ambaye alikuwa akipewa onyo mara kwa mara kutokana na kumkumbatia Cheka na kukosa pumzi. Matokeo ya mabondia hao walizidiana kwa pointi chache, ambapo majaji watatu wa pambano hilo walikuwa ni John Chabu, Boniface Wambura na Malk Hatiya, ambapo pointi zao zilikuwa kwa jaji wa kwanza hadi wa tatu kwa upande wa Nyilawila walitoa pointi 96, 97 na 97 ambapo kwa Cheka pointi zilikuwa 100, 99 na 99. Pambano la mabondia Nyilawila na Cheka lilitanguliwa na mapambano ya utangulizi kutoka kwa mapondia Seba Temba wa Morogoro dhidi ya Ibrahimu Mwakalolo wa Dar es Salaam na Temba alimshinda Mwakalolo. Pambano lingine la utangulizi lililokuwa la ushindani mkubwa ni kati ya Nassib Ramadhan wa Morogoro na Antony Mwapalili wa jijini Dar es salaam na ushindi ulienda kwa Nassib ambaye alishinda kwa pointi 180 kwa pointi 170. Mratibu wa pambano hilo, John King alisema kuwa huo utakuwa muendelezo wa kuandaa mapambano, kwa sababu mchezo wa ngumi una mashabiki wengi. |



Lilian Lucas,Morogoro










