MwanzoContactsEmail
Home Michezo Ngumi Matumla amfunika Maneno Oswald
BOOKMARK THIS PAGE
Matumla amfunika Maneno Oswald  Send to a friend
Tuesday, 31 January 2012 21:45

Imani Makongoro
BONDIA, Rashid 'Snake man' Matumla amemfunika Maneno Oswald katika viwango vya ubora Tanzania na duniani.
Kwa mujibu wa mtandao wa ngumi wa dunia 'Boxrec' Matumla anashika nafasi ya tano kwa ubora hapa nchini akiwa na pointi 10 zaidi ya mpinzani wake.

Rekodi hizo zinaonyesha Maneno mwenye pointi 7 akiwa nafasi ya 6 huku katika viwango vya dunia Matumla ameendelea 'kumburuza' Maneno baada ya kushika nafasi ya 229 na Maneno 258.

Mtandao huo ulibainisha kuwa Francis 'SMG' Cheka ndiye bondia bingwa hapa nchini akiwa na ponti 66 huku akishika nafasi ya 70 duniani akifuatiwa na Kalama Nyilawila mwenye pointi 57 akiwa kwenye nafasi ya 78 duniani.

Nafasi ya tatu kwa ubora ilichukuliwa na Mada Maugo ambaye alipata pointi 38 na Benson Mwakyembe mwenye pointi 23 akishika nafasi ya nne mbele ya Matumla aliyefunga pazia la tano bora hiyo ya Tanzania.

Nafasi ya saba hadi ya kumi zilichukuliwa na Said Mbelwa (5) , Bagaza Mwambene (2) huku Yusuph Jibaba na Kaminja Ramadhan wakiwa hawana pointi licha ya kukamilisha 10 bora hiyo ya Tanzania kutokana na mapambano waliyocheza.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner