
| Chipukizi tenisi hao Burundi | Send to a friend |
| Monday, 02 January 2012 21:45 |
|
TIMU ya taifa ya vijana wa Tanzania itaondoka kesho kuelekea Burundi na wachezaji 11 tayari kushiriki mashindano ya kanda ya Afrika Mashariki yaliyopangwa kuanza Januari 8-18. Akizungumza na Mwanainchi jana kocha wa timu hiyo Hassani Kasimu alisema mashindano hayo yameandaliwa ITF kwa ajili ya kuchagua wachezaji watakaoshiriki katika mashindano ya Afrika Jounior championship nchini Bostwana. Hassan alitaja wachezaji watakaoshiriki kwa upande wa umri wa miaka 16 ni John Njau, Goodluck Shelemo, Edna John na Zuhura Baraka. Upande wa umri wa miaka 14 ni Sara Bura,Tumaini Martin, Rahabu Shabani na Emanuel Nicodemu na umri wa miaka 12 watakuwepo Abu Hamisi, Asia Morisi na Omary Sulle. Alisema kati ya wachezaji hao vijana wawili Emanuel Nicodem na Omary Sulle wako nchini Burundi katika kituo cha mafunzo cha mchezo wa tenisi kinachosimamiwa na ITF. Mwaka jana vijana waliofuzu na kushiriki katika mashindano ya Afrika Jounior championship walikuwa Tumain Martin, Edna John na Lydia Lucas.Nchi zinazotarajia kushiriki ni Kenya, Uganda Ethiopia,Tanzania, Rwanda, Burundi, Somalia na Shelisheli. |
| Last Updated on Monday, 02 January 2012 21:50 |














