
| RBA yaanza leo | Send to a friend |
| Friday, 06 January 2012 19:36 |
|
PAZIA la ligi ya mpira wa kikapu mkoa Dar es Salaam (RBA) litafunguliwa leo kwa kuzikutanisha JKT dhidi ya ABC kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa jijini hapa. Mchezo wa leo unatarajia kuwa mkali na kuvutia kutokana na historia za timu hizo zinavyokutana kwenye mashindano mbalimbali. Timu ya JKT ikiwa na nyota wake kama Himidi choka, Frank Kusiga, Francis Mlewa, Frank Simkoko na Charles Makene watashuka kwa lengo moja tu la kusaka ushindi muhimu. Matumaini ya ABC kwenye mchezo huo ni mchezaji bora wa mashindano ya Taifa Cup, Filbert Mwaipungu atakayekuwa akisaidiwa na Adamu Jegame na Gilbert Batungi. Akizungumza jana kocha wa ABC, Leonard Kwale alisema anategemea mchezo utakuwa mgumu kwao, lakini watapambana hadi dakika ya mwisho. Mbali ya mechi hiyo mechi nyingine itakayofanyika kesho itawakutanisha Savio na Polisi, kwa upande wanawake timu ya Lady Lioners itacheza na Vijana Queen. Mgeni rasmi katika ufunguzi wa leo anategemea kuwa Mbunge wa wilaya ya Temeke, Abas Mtemvu ambapo baadaye chama cha mchezo wa kikapu kinatarajia kumtangaza kuwa mlezi wa kikapu kwa mkoa wa Dar es Salaam. Baadhi ya timu zinazoshiriki katika mashindano hayo ya RBA ni Savio, ABC, Hoope Life, Vijana, JKT, Magone, Chui na Pazi |














