MwanzoContactsEmail
Home Michezo Michezo Mingine Taifa Queens yaloa kwa Zambia
BOOKMARK THIS PAGE
Taifa Queens yaloa kwa Zambia  Send to a friend
Monday, 09 January 2012 21:00

Jackson Odoyo, Zanzibar
TIMU ya Taifa ya netiboli, Taifa Queens jana ilipoteza matumaini na kubakiza Kombe la Mapinduzi nyumbani baada ya kukubali kipigo cha magoli 44-41 kutoka kwa  Zambia.

Taifa Queens ilionekana kuzidiwa kiufundi na Zambia waliokuwa makini kwenye kutumia nafasi walizopata na kutopeza pasi zao.

Katika mchezo huo uliokuwa wa vuta ni kuvute ulianza kwa mfungaji wa Taifa Queens, Mwanaidi Hassan alikosa magoli manne ya mwanzo na kuwafanya Wazambia kumaliza robo kwanza wakiwa mbele kwa magoli 10-8.

Katika kipindi cha pili, Taifa Queens walijipanga ipasavyo ambapo kocha Mary Protase alimtoa mlinzi Jacqulini Shemeza na kuingiza Siwa Juma na kuimarisha safu ya ulinzi.

Katika robo ya tatu Queens walicheza vizuri na kufanikiwa kufunga magoli ya haraka kupitia Asha  Ibrahim aliyeamua kufunga kutoka mbali na kuwafanya walinzi wa Zambia wasijue la kufanya.

Tanzania ilimaliza robo hiyo ikiwa mbele kwa magoli 38-35. Robo ya mwisho ilianza kwa kasi kwa timu zote mbili kushambuliana kwa zamu na kuwindana ambapo Wazambia walikuwa makini zaidi na kutunza pasi zao huku Taifa Queens ikizipoteza hivyo kuwapa wageni hao nafasi ya ushindi.

Hii ni mechi ya pili mfululizo wa timu ya Tanzania kufungwa na imebaki na mechi moja dhidi ya Kenya itakayochezwa Alhamis katika viwanja vya Gymkhana.

Zambia imeshinda mechi zake zote mbili na kesho ni mapumziko ambapo Jumatano  timu ya Taifa ya wanaume itacheza na Uganda.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner