MwanzoContactsEmail
Home Michezo Michezo Mingine Ikangaa huyo AT
BOOKMARK THIS PAGE
Ikangaa huyo AT  Send to a friend
Tuesday, 31 January 2012 21:47

Imani Makongoro
MSHINDI wa medali ya Fedha ya michezo ya Jumuiya ya Madola ya mwaka 1982 katika mbio za Marathon (km 42), Juma Ikangaa ametangaza nia ya kuwania urais wa Chama cha Riadha Tanzania (AT).

Mbali na Ikangaa, pia mshindi wa medali ya fedha ya Olimpiki 5000 mwaka 1980, Suleiman Nyambui ametangaza nia yake ya kuendelea kutetea nafasi ya Katibu Mkuu katika uchaguzi utakaofanyika Machi 17 mjini Songea, Ruvuma.Katika uchanguzi huo unaotegemewa kuwa na upinzani mkali tayari wagombea watatu wamejitokeza kuwania nafasi ya rais.

Wagombea waliojitokeza kuwania uongozi huo katika nafasi ya rais ni Francis John anayetetea kiti chake, Henry Ng'itu na Ikangaa Katibu Mkuu wa zamani wa AT.

Kwa upande wa Katibu Mkuu, Nyambui anategemea kupata upinzani kutoka kwa John Manyama baada ya John Bayo kujiengua kwenye kinyang'anyiro hicho.Katika nafasi ya makamu wa rais, hadi sasa Hamad Ndeya ndiye anayetetea nafasi yake.

Nafasi nyingine zinazowaniwa ni ile ya wajumbe 10 wa kamati ya utendaji ya AT na ile ya mweka hazina inayoshikiliwa na Morice Okinda.Katika hatua nyingine AT imefungua milango kwa wadau wa mchezo huo kutoka visiwani Zanzibar kuwania uongozi huo wa chama hicho.

Fomu za kuwania nafasi mbalimbali za chama hicho zinatolewa kuanzia leo kwenye ofisi za AT na Baraza la Michezo la Taifa jijini Dar es Salaam kwa Tsh 20,000.

Kabla ya uchaguzi huo utafanyika Mkutano Machi 16 mjini Songea.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner