
| AC Milan kuwaaa Juve | Send to a friend |
| Saturday, 28 January 2012 09:20 |
|
MILAN, Italia Katika muda wa dakika nne, Milan walikwamisha wavuni mabao mawili kupitia Robinho na Seedorf, kabla ya mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden, Zlatan kukamilisha ushindi kwa kufunga bao la tatu. Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil, Robinho alifunga bao lake kwa shuti kali la karibu na lango baada ya dakika 15 tangu kuanza mchezo likiwa bao la kusawazisha, na kiungo Seedorf aliipeleka mbele Milan kwa kufunga bao la pili baada ya kumuadaa kipa Federico Marchetti na kupiga shuti lililokwenda wavuni. Ibrahimovic alikamilisha ushindi kwa kufunga bao la tatu dakika sita kabla ya mchezo kumalizika. Juventus waliichapa AS Roma mabao 3-0 Jumanne iliyopita, huku Napoli wakiwatupa nje ya mashindano waliokuwa mabingwa watetezi, Inter Milan kwa kuichapa mabao 2-0 na Siena wakiiondoa Chievo Verona kwa bao 1-0. |













