
| Louis saha atua rasmi Tottenham | Send to a friend |
| Thursday, 02 February 2012 08:11 |
|
LONDON, England Wakati Redknapp akimsajili Saha, pia imemruhusu Roman Pavlyuchenko kuondoka na kwenda kujiunga na klabu ya Lokomotiv Moscow ya nchini Russia.Redknapp aliwaambia waandishi wa habari: "Ni mkataba wa kudumu, lakini si wa muda mrefu. Nampenda Louis Saha, naheshimu kiwango chake. "Kwangu, namchukulia kama mchezaji mwenye uwezo na anaweza kufunga magoli. Amefanya makubwa Everton, lakini mwishoni mwa mwaka mkataba wake utalamizika."Nao QPR walitumia siku ya mwisho ya zoezi la usajili dirisha dogo kumsajili mshambuliaji Bobby Zamora kutoka klabu ya Fulham kwa mkataba wa miaka minne na nusu. Ada ya uhamisho ya nyota huyo inadhaniwa kufikia paundi 4.5milioni na mambo yalikamilika saa chache kabla ya saa sita usiku Jumanne wiki hii.Zamora ataungana na kocha mpya, Mark Hughes ambaye alishawahi kufanya naye kazi kwenye Uwanja wa Craven Cottage. Aidha, ataungana pia na Djibril Cisse, aliyekwenda dimba la Loftus Road akitoka Lazio kwa ada ya uhamisho ambayo haijawekwa wazi.Fulham walikuwa tayari kumtoa mshambuliaji huyo baada ya kumsajili mshambuliaji wa Stuttgart, Pavel Pogrebnyak kwa mkataba wa miezi sita. Klabu ya Everton imemsajili kwa mara ya pili kiungo Steven Pienaar kutoka Tottenham. Mchezaji huyo amesajiliwa kwa mkopo mpaka mwishoni mwa msimu. Klabu hiyo imesajili Pienaar, huku pia mshambualiaji wake Louis Saha akienda kujiunga na Spurs. Aidha, Manchester City wamekamilisha uhamisho wa kiungo David Pizarro kutoka Roma ambaye atacheza kwa mkopo mpaka mwishoni mwa msimu. Pizarro, 32, mchezaji wa kimataifa wa Chile amecheza mara saba tu kwenye kikosi cha Roma katika mechi za Ligi Kuu Italia. Kabla ya kujiunga na Roma na kisha kuja City, alicheza Inter Milan ambayo wakati huo ilikuwa ikifundishwa na kocha Roberto Mancini. Mancini alisema: "Pizarro ni mchezaji mzuri. Nadhani anaweza kutusaidia katika miezi mitatu ijayo kwa sababu ni mchezaji mzuri." Pizarro aliyeshinda mataji matatu--Kombe la Super, Coppa Italia na ubingwa wa Italia msimu wa mwaka 2005-06 akiwa Inter. |














