MwanzoContactsEmail
Home Michezo Michezo ya Kimataifa Man United yaikamata Man City kileleni
BOOKMARK THIS PAGE
Man United yaikamata Man City kileleni  Send to a friend
Thursday, 02 February 2012 08:13

LONDON, England
USHINDI wa mabao 2-0 waliopata Manchester United dhidi ya timu ya Stoke umewafikisha pointi sawa na mahasimu wao, Manchester City waliokuwa na usiku mbaya juzi baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 toka Everton.Hata hivyo, Manchester City inaendelea kuongoza msimamo wa Ligi wa tofauti za hesabu ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Shujaa wa Everton kwenye Uwanja wa Goodison Park alikuwa mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Darron Gibson aliyefunga bao pekee kwenye mechi hiyo.

City walicheza vizuri kipindi cha kwanza kwa kufanya mashambulizi ya mara kwa mara, huku mshambuliaji Samir Nasri akishindwa kufunga baada ya shuti lake kugonga mwamba.

Kulikuwa na tukio la shabiki kuvamia uwanjani na kwenda kwenye lango la kipa Joe Hart kabla watu wa usalama kwenda kutoa na kusababisha mpira kusimama kwa dakika nne mwishoni mwa kipindi cha kwanza.

Gibson alifunga hilo kwa shuti kali akiwa umbali wa mita 20 lililombabatiza Gareth Barry na kujaa wavuni.
Juhudi za City kutaka kusawazisha bao hilo hazikufanikiwa mpaka mwisho wa mchezo.

Manchester United ilirejea kwa kishindo toka kuondolewa kwenye michuano ya Kombe la FA na juzi usiku walitumia vizuri Uwanja wao wa Old Trafford kuifunga Stoke City.

Katika mechi hiyo, United haikucheza vizuri pamoja na kuibuka na ushindi, huku ikifunga bao la kwanza likifungwa kwa mkwaju wa penalti na mshambuliaji Javier Hernandez.

Penalti hiyo ilitolewa baada ya Jermaine Pennant kumchezea vibaya Park Ji-sung ndani ya eneo la hatari.
United ilijihakikishia ushindi kwa kufunga bao la pili nalo likija kwa njia ya kiki ya penalti, safari hii likifungwa na Dimitar Berbatov kufuatia Jonathan Walters kumuangusha ndani ya eneo la hatari  Antonio Valencia.
Tottenham iliendelea kuimarisha 'presha' kwa Man United na Man City kileleni mwa msimamo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 kwenye uwanja wao wa nyumbani dhidi ya Wigan.

Gareth Bale alikuwa wa kwanza kuziona nyavu za Wigan baada ya kupokea pasi ya Luka Modric na kuukwamisha wavuni mpira, kabla ya muda mfupi baadaye Modric kuongeza bao la pili akifunga kwa shuti kali la mita 20.
Alikuwa Bale aliyeng'ara kwenye mechi hiyo alipofunga bao la tatu kwa kiki iliyoshindwa kuchezwa na kipa James McArthur. McArthur alifunga bao pekee la kufutia machozi kwa Wigan.

Goli la kujifunga mwenyewe la mchezaji Neil Taylor katika sekunde za majeruhi, lilitosha kuzipa sare ya bao 1-1 Chelsea na Swansea kwenye Uwanja wa Liberty.

Mchezaji wa zamani wa Chelsea, Scott Sinclair alikuwa wa kwanza kufunga bao kwa Swansea kabla ya bao la kujifunga wenyewe Taylor.Katika mechi hiyo, Chelsea walilazimika kucheza pungufu baada ya  Ashley Cole kuonyesha kadi ya pili ya njano kwa kosa la kumchezea vibaya Nathan Dyer.

Hata hivyo walicheza kwa nguvu na kufanikiwa kusawazisha bao baada ya mkwaju mkali wa Jose Bosingwa kumbabatiza Taylor na kujaa wavuni zikiwa zimesalia sekunde tu mchezo kumalizika.

Liverpool nayo ilipata ushindi wa pili katika mechi saba baada ya kuifunga Wolves mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Molineux.

Mchezaji Andy Carroll alikufunga bao lake la kwanza Ligi Kuu tangu ajiunge na Liverpool Januari mwaka jana.
Carroll alifunga bao hilo katika kipindi cha pili baada ya mechi 12 za Ligi Kuu akimalizia wavuni kwa shuti kali pasi ya Charlie Adam.Craig Bellamy aliongeza bao la pili kabla ya Dirk Kuyt kufunga bao la tatu.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner