MwanzoContactsEmail
Home Michezo Michezo ya Kimataifa Ronaldinho ang'ara
BOOKMARK THIS PAGE
Ronaldinho ang'ara  Send to a friend
Thursday, 02 February 2012 21:46

RIO DE JANEIRO, Brazil
KIUN GO Ronaldinho alifunga bao moja na kutengeza jingine na kuisaidia Flamengo kuichapa timu ya Bolivia, Real Potosi 2-0 na kufuzu kwa hatua ya makundi ya Copa Libertadores kwa jumla ya mabao 3-2.

Internacional ya Brazil pia ilifuzu kwa 3-2 baada ya kulazimisha sare 2-2 na Once Caldas ya Colombia.

Ronaldinho alipiga mpira wa adhabu na kuunganishwa kwa kichwa na Leonardo Moura dakika ya 39 kwenye Uwanja wa Engenhao, kufanya mchezo huo kuwa 2-2 na kuiwezesha Flamengo kuwa mbele kwa goli la ugenini.

Mchezaji bora mara mbili wa FIFA wa mwaka wa zamani alifunga bao la ushindi dakika za mwisho, alipowalamba chenga mabeki na kupiga shuti lililokwenda moja kwa moja wavuni.

“Tumepata mabao sahihi ya kutuwezesha kufuzu kwa hatua ya pili,” alisema Ronaldinho.

Flamengo inaungana na timu ya Argentina, Lanus,  Olimpia(Paraguay) na Emelec (Ecuador), katika Makundi 2 ya mashindano hayo makubwa ya klabu ya Latin Amerika.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner