MwanzoContactsEmail
Home Michezo Michezo ya Kimataifa Newcastle yapaa, Arsenal yaporomoka
BOOKMARK THIS PAGE
Newcastle yapaa, Arsenal yaporomoka  Send to a friend
Thursday, 02 February 2012 21:47

LONDON, England
NEWCASTLE United imekaribia nne bora iliposhinda 2-0 dhidi Blackburn Rovers, huku Arsenal ikiporomoka hadi nafasi ya saba baada ya kulazimishwa suluhu na Bolton Wanderers katika Ligi Kuu.

Bao la kujifunga Scott Dann na lile la pili lililofungwa na Gabriel Obertan kumeipasha Newcastle hadi nafasi ya tano, pointi tatu nyuma ya  Chelsea, huku Rovers wakirejea kwenye mstari wao wa kushuka daraja.

Arsenal ilipata sare na Bolton na kubaki pointi tano nyuma ya timu zilizokuwa kwenye nne bora nafasi ambayo walikuwa wakijihakikisha muhongo uliopita chini ya kocha Arsene Wenger aliyeshudia mshambuliaji wake Robin van Persie mara mbili akigongesha mwamba.

“Tunaimani, tunahamu na tunajiamini. Tumepita kwenye kipindi kigumu na tunatakiwa kupambana na hilo, lakini tupo tayari kwa ushindani,” alisema Wenger wakati alipoulizwa kuhusu nafasi ya timu yake kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

“Tunamatumaini kuwa tutaendelea kupambana na hatutopoteza kujiamini kwetu.”

Djibril Cisse alihitaji dakika15 kuthibisha kurejea kwake katika Ligi Kuu alipofunga bao lake la kwanza kwa Queen’s Park Rangers ilipotoka sare  2-2 na Aston Villa.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 30, aliwahi kuichezea Liverpool na Sunderland, alisajili siku ya usajili akitokea Lazio, alipiga shuti kali lililomshinda kipa wa Villa, Shay Given.

QPR ilipata bao la pili kupitia kwa Stephen Warnock aliyejifunga, lakini mshambuliaji Darren Bent na Charles N’Zogbia walisawazisha kwa Villa.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner