
| Kipigo cha mkimbiza kocha Ahly | Send to a friend |
| Saturday, 04 February 2012 09:08 |
|
KOCHA wa Al-Ahly, Manuel Jose, amerudi kwao Ureno ili kukwepa vurugu zinazoendelea nchini Misri. Kocha huyo alisema kuwa alilazimika kuondoka kufuatia kupata hofu kubwa baada ya kuona watu walivyokuwa wakiuana kwenye mechi kati ya Al-Ahly na Al Masry katikati ya wiki hii. Vile vile kocha huyo alisema kuwa alijikuta akipigwa ngumi na marungu bila kutarajia, jambo ambalo limemsababishia maumivu makali. Katika tukio hilo lililotikisa soka ya dunia, watu 74 walifariki. Nchini Misri waandamanaji wamerejea katika mitaa ya mji mkuu Cairo kuonyesha hasira yao juu ya maisha ya mashabiki 75 yaliyotokea uwanjani. Kwenye kikao cha dharura cha bunge, Waziri mkuu wa nchi hio ametangaza kua wanakamati wa Chama cha mpira cha nchi hiyo wote wamefutwa kazi na wanachunguzwa. Gavana wa mji wa Port Said amejiuzulu. Waziri Mkuu wa Misri, Kamal Ganzouri ametangaza hatua ya kuwafuta kazi wanachama wote wa chama cha mpira cha Misri na kujizulu kwa baadhi yao kwenye kikao cha dharura cha Bunge. Hatua hiyo huenda isitoshe kuwaridhisha Wamisri wengi. Kuna dalili la kuongezeka kwa ghadhabu ya wa Misri juu ya Wizara ya mashauri ya nchini inayosimamia Polisi, ambayo wengi wanahisi haijabadilika tangu enzi za Hosni Mubarak. Na ghadhabu hizo zimemuelekea kiongozi wa Misri wa kijeshi Field Marshall Tantawi. Mashabiki wa klabu ya Al Ahli, ambao wenzao walishambuliwa mjini Port Said, wameanza safari ya miguu kuelekea medani ya Tahrir na makao ya Wizara ya masuala ya ndani. Wabunge kutoka chama cha Muslim Brotherhood wanaongoza katika kuikashifu serikali bungeni. Kila mmoja anahofia kua huenda haya yakazua duru mpya ya malumbano ya mitaani. Pamoja na hayo, hali hii inazidi kupunguza matumaini ya mchakato wa mageuzi ya utawala kutoka mikononi mwa Wanajeshi na kukabidhiwa raia. |














