
| City yaiombea mema Chelsea kwa Man United | Send to a friend |
| Saturday, 04 February 2012 09:10 |
|
BAADA ya kuduwazwa katikati ya wiki Manchester City leo watakuwa na nafasi ya kujiuliza tena wakati watakaposhuka dimbani kuikabili Fulham. Kipigo cha kushangaza cha bao 1-0 kutoka kwa Everton pamoja na ushindi wa Manchester United 2-0 dhidi ya Stoke City kumezifanya timu hizo kuongoza kwa pointi 54, tano zaidi ya Tottenham Hotspur inayoshika nafasi ya tatu. Hata hivyo, ratiba ya wiki hii inatoa hafueni kidogo kwa City ambao wameuanza mwaka 2012 kwa kishindo. United itakuwa na kibarua dhidi ya Chelsea hapo kesho kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, uwanja ambao hawajawahi kushinda kwa miaka 10 iliyopita, huku Tottenham watakuwa wageni Anfield siku ya Jumatatu kuivaa Liverpool iliyozaliwa upya pia wakiongezwe nguvu kwa kurejea kwa Luis Suarez aliyemaliza kifungo cha mechi nane. City wanaonekana wameshindwa kabisa kuziba pengo la Yaya Toure ambaye bado yuko kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika akiwa na Ivory Coast, wameshinda mechi zote 11 za ligi walizocheza nyumbani msimu huu huku Fulham wamefanikiwa kushinda mechi moja tu ugenini. Hakuna jingine zaidi ya pointi tatu kwa vijana Roberto Mancini ili kuongoza kwa tofauti pointi hizo kwa saa 24, lakini kocha wa United, Alex Ferguson hataka kuachwa kwa pointi zaidi, ushindi ndicho kitu anachokitaka kwa kila nafasi itakapopatikana. “Labda nilifikiri kabla ya mchezo kwamba itakuwa mechi rahisi,” alisema Mancini baada ya kipigo cha Goodison Park. “Sitaki jambo hilo lijirudie tena leo. Najiraumu kwa makosa yanguI.” Mancini ataweza kumtumia David Pizarro kwenye mchezo huo dhidi Fulham baada ya kumsajili kiungo huyo wa Chile kutoka AS Roma. Pizarro, aliyekuwa na Mancini pale Inter Milan wakati walipotwaa ubingwa wa Italia 'Scudetto' mwaka 2006, hata hivyo hajapata nafasi ya kucheza muda mwingi msimu huu, lakini anaamini ataweza kuwasaidia City kupata ushindi. “Ni nafasi ya pekee kuingia kwenye historia ya klabu hii, lengo langu ni kuisaidia klabu hii kutwaa taji la Ligi Kuu msimu huu,” Pizarro alilimbia gazeti la Manchester Evening. United haijashinda kwa Chelsea katika mechi ya ligi tangu mwaka 2002, lakini klabu hiyo ya London imepoteza mwelekeo wakiwa nafasi ya nne na Stamford Bridge si sehemu ya kutisha tena. Chelsea itashuka dimbani bila ya beki wake wa kushoto Ashley Cole, aliyepewa kadi nyekundu walipotoka sare 1-1 na Swansea City Jumanne iliyopita, na Ferguson anajiamini kuwa timu yake itavunja mwiko wa kushinda magharibi mwa London na kuendelea kuipa presha City. “Mechi dhidi ya Chelsea katika miaka ya karibuni imekuwa ngumu kwetu na bahati mbaya tumekuwa tukipata matokeo yasiyoridhisha,” aimbia tovuti ya United (www.manutd.com) “Wachezaji wanajua nini cha kufanya. Tumekuwa na matokeo mazuri ugenini msimu huu na tunahitaji kuendelea na kasi hiyo. “Tunacheza mechi muhimu zote ugenini dhidi Chelsea, Tottenham na City. Zitakuwa ni mechi ngumu.” TUMAINI LA UBINGWA Tottenham imerudisha matumaini ya ubingwa kwa ushindi wake wa mabao 3-1 dhidi ya Wigan Athletic na ushindi wa mechi mbili za ligi dhidi ya Liverpool msimu uliopita inamaanisha vijana wa Harry Redknapp watashuka dimbani Jumatatu kwa kujiamini zaidi. Timu hiyo ina majeruhi wachache kama winga wake Aaron Lennon, washambuliaji Jermain Defoe, Rafael van der Vaart na kuna uwezekano wasiwepo siku hiyo. Kocha Harry Redknapp pia anapamba na mchezo huo huku akiwa na kesi mahakamani akidaiwa kukwepa kulipa kodi. Liverpool iliyo nafasi ya sita hawana shaka hiyo baada ya kurejea kwa Suarez na Andy Carroll kufunga waliposhinda 3-0 dhidi ya Wolverhampton Wanderers siku ya Jumanne. Hilo ni bao la kwanza kwa Carroll katika ligi tangu mwezi Oktoba na kuthibisha kwanini Liverpool walitoa dola 55 milioni kumsajili kutoka kwa Newcastle United mwaka moja uliopita. Wakiwa nafasi ya tano, Newcastle wanaweza kuweka pabaya Chelsea kama wakishinda mechi yao ya mchana kesho dhidi ya Aston Villa huku Arsenal wakiwa nafasi ya saba, wanamatumaini ya kurejea kwenye mstari wa ushindi nyumbani dhidi Blackburn Rovers leo. |














