
| Zidane aitwa kuiokoa Ufaransa | Send to a friend |
| Thursday, 02 September 2010 21:37 |
CLAIREFONTAINE, UfaransaKIUNGO wa zamani wa Ufaransa, Zinedine Zidane juzi aliunganisha nguvu na kocha, Laurent Blanc kujenga morali ya wachezaji iliyopotea baada ya Fainali za Kombe la Dunia mwaka huu. Zidane alikutana na wachezaji kwenye mji wa Clairefontaine na walikuwa wakiangalia mkanda jinsi Ufaransa ilivyotwaa Kombe la Dunia 1998 na lile la Ulaya 2000. Ufaransa itacheza na Belarus leo kabla ya kwenda Bosnia Jumanne kwa ajili ya mechi za kufuzu Euro 2012. “Nawatakia kila la kheri katika siku za kwanza za maandalizi yao,” alisema Zidane, ambaye aliwatembelea Clairefontaine kwa mara ya mwisho walipokuwa wakijiandaa kwa Fainali za 2006. “Ni wachezaji wapya, wazuri wanaoweza kutuunganisha lakini inatakiwa wajitambue na watambue majukumu yao ya uwanjani.” |



CLAIREFONTAINE, Ufaransa









