Bifu la Kanye na Drake laanza upya

Muktasari:

  • Kanye wakati akifanya mahojiano na podcast ya ‘The Download’ amedai kuwa Drake ameenda kinyume na Mungu anavyotaka, kwa kukabidhi nafsi yake kwa shetani ili agombane na yeye.

Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu wanamuziki wa Marekani Kanye West na Drake wamerudisha tena bifu lao baada ya Kanye kudai kuwa rapa huyo amekabidhi nafsi yake kwa shetani ndiyo maana anamsema.

Kanye wakati akifanya mahojiano na podcast ya ‘The Download’ amedai kuwa Drake ameenda kinyume na Mungu anavyotaka, kwa kukabidhi nafsi yake kwa shetani ili agombane na yeye.

Inadaiwa kuwa bifu la wawili hao linatokana na ushindani wao katika muziki huku kila mmoja akitaka kuonekana bora kuliko mwenzie ambapo hivi karibu Kanye ameachia wimbo uitwao ‘Like That’ aliomshirikisha Metroboomin, ukidaiwa kuwa ni dongo kwenda kwa Drake.

Ikumbukwe kuwa mwaka 2021 wawili hao walikuwa kwenye bifu kama hilo, lakini Desemba mwaka huo walimaliza bifu lao na kufanya tamasha la pamoja nchini humo.