Diamond awapa ushauri wasanii wa Bongo Fleva

Muktasari:

  • Hata hivyo, ameeleza kuwa kwa upande wa wasanii wote waliopita mikononi mwake ambao ni Harmonize na Rayvanny kwa sasa anaongea nao vizuri huku akidai kuwa ataendelea kuishi nao vizuri kwa sababu wanapofanya vizuri na kupata krediti lazima na yeye atajwe.

Mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini Diamond Platnumz, leo Machi 11, wakati akizungumzia na waandishi wa habari amewataka wasanii wa Bongo Fleva kuacha kushindana kwa vitu visivyo na maana kwenye mitandao ya kijamii badala yake waanze kushindana  kutoa kazi bora.

Hata hivyo, ameeleza kuwa kwa upande wa wasanii wote waliopita mikononi mwake ambao ni Harmonize na Rayvanny kwa sasa anaongea nao vizuri huku akidai kuwa ataendelea kuishi nao vizuri kwa sababu wanapofanya vizuri na kupata krediti lazima na yeye atajwe.

Aidha mwanamuziki huyo pia alizungumza machache kuhusiana na sakata linalomkabili mkali wa Hip-Hop nchini Marekani Diddy na kueleza kuwa hawezi kumjaji kwa chochote kwani aliwahi kukutana naye na kuzungumza naye, licha ya yote yanayomkabili lakini anamuheshimu.