Huyu ndiye Diddy, anayeandamwa na tuhuma za unyanyasaji wa kingono

Muktasari:

  • Diddy alianza kufanya kazi ya muziki kama mwongozaji katika lebo ya 'Uptown record' kabla hajaanzisha lebo yake ya 'Bad Boy Record' mwaka 1993 alipowasajili baadhi ya wasanii katika kama The Notorius B.I.G, Mary J.Blige na Usher Raymond.

Sean John Combs ndiyo jina lake halisi alilopewa na wazazi wake. Alizaliwa Novemba 4 mwaka 1969, New York Marekani mama yake aliitwa Janice Combs, alikuwa ni mwalimu na mwanamitindo, baba yake aliitwa Melvin Combs alikuwa mhudumu wa Jeshi la U.S Air Force, aliuwawa mwaka 1972, kwa risasi ndani ya gari, P Diddy akiwa na umri wa miaka miwili.      

                      

                     Picha ya Diddy akiwa na wazazi wake

Diddy alianza kufanya kazi ya muziki kama mwongozaji katika lebo ya 'Uptown record' kabla hajaanzisha lebo yake ya 'Bad Boy Record' mwaka 1993 alipowasajili baadhi ya wasanii katika kama The Notorius B.I.G, Mary J.Blige na Usher Raymond  

                       

                       

                   Picha ya pamoja Diddy akiwa na mama yake

Diddy amebahatika kupata watoto saba kwa wanawake tofauti, watoto hao ni Quincy,Justin, King, Chance, Love na mapacha Dlila na Jessie     

             

                        

                                  Diddy akiwa na wanaye

         

Hivi karibuni kumekuwa na shutuma nyingi juu ya nyota huyo ambazo zilianza kuibuka mapema mwaka jana, tunaweza kusema 2023 na 2024, siyo miaka mizuri kwa Diddy, kutokana na tuhuma za unyanyasaji wa kingono alizokutana nazo mwanamuziki huyo.

Hadi kufika mwaka huu 2024, wanawake wanne tayari wamemshutumu Diddy kwa kuwafanyia vitendo hivyo. Licha ya kuwa wanasheria wake na yeye mwenyewe hakuwahi kukubaliana nazo, jana Jumatatu, Machi 25 yaliibuka mapya baada ya makazi yake ya Los Angeles na Miami kufanyiwa upekuzi na Mawakala wa Usalama wa Taifa kama sehemu ya uchunguzi wa serikali kuhusu madai ya biashara ya ngono yanayomhusisha msanii huyo.

Uchunguzi huo uliongozwa na mawakala wa Uchunguzi wa Usalama wa Nchi (HSI). Tuhuma za unyanyasaji wa kingono zinazomkabili Diddy ni zile zilizoanza kuvuma tangu mwaka jana.

Hata hivyo, katika upekuzi huo, watoto wawili wa kiume wa Diddy, Justin na King Combs, walitiwa mikononi mwa askari.  Jumba lililofanyiwa upekuzi ni lile ambalo alizindulia albamu yake ya mwisho mwaka jana (The Love Albam Off the Grid).

Utakumbuka kuwa mpenzi wa zamani wa Diddy, Casandra Ventura, maarufu kwa jina Cassie, aliwahi kumshutumu staa huyo kwa kumbaka na kumshambulia mara kwa mara na kusema alimlazimisha kufanya mapenzi na wanaume mbele yake.

                       

                        

     Diddy akiwa na  mpenzi wake wa zamani Casandra Ventura


Pia Joi Dickerson-Neal, alimshutumu Diddy kwa kumpa dawa za kulevya na kumbaka mwaka wa 1991. Na mwanamke aliyetambulika kwa jina la Jane Does mwaka jana alifungua kesi akimtuhumu Diddy kuwa alishirikiana na wenzake kumfanyia ukatili wa kingono mwaka 2003, wakati akiwa na miaka 17 huku Diddy akiwa na miaka 34. Si hivyo tu zipo tuhuma nyingine pia za unyanyasaji wa kingono zinazomkabili nyota huyo.

Hata hivyo, baada ya kudakwa kwa watoto wake vyombo vya habari mbalimbali nchini Marekani vilidai kuwa mwanamuziki huyo tajiri amekimbilia katika Visiwa vya Caribbean, baada ya kuonekana katika Uwanja wa Ndege wa Opa-Locka. Lakini madai hayo yamekanushwa na jarida la 'People' kwa kudai kuwa Diddy bado yupo Marekani, na hakuwepo kwenye ndege hiyo inayodaiwa aliondoka nayo.

Taarifa hiyo inakuja baada ya ndege binafsi ya Diddy kuonekana ikifanya safari za mara kwa mara toka juzi Jumapili huku safari yake ya mwisho ikiwa ni katika kisiwa hicho cha Caribbean.

Aidha hadi kufikia sasa bado haijabainishwa ni wapi msanii huyo yupo licha ya watoto wake hao wawili kukamatwa na askari.