Wakaguzi hesabu 75 wapata kazi UN

Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Tanzania,Ludovick Utoh

Wakaguzi 75 wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali (Naot), wataondoka nchini mwishoni mwa mwezi huu kwenda nchi mbalimbali kufanya ukaguzi wa hesabu za mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN). Mwaka 2011, Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh aliteuliwa kuwakilisha Afrika kuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakaguzi wa Hesabu za UN na kwamba, moja ya majukumu ya Naot ni kufanya ukaguzi katika mashirika ya umoja huo. Akizungumza mjini Bagamoyo jana, Utouh aliwataka kufanya kazi kwa kufuata maadili ya kazi yao. (Raymond Kaminyoge)